WIZARA YA AFYA YAKABIDHIWA HOSPITALI YA MKOA YA MAWENI

4-01
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akimkabidhia Mhasibu Mkuu wa Wizara ya afya Hellen Mwakipunda ripoti hiyo
  • Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhiwa rasmi hospitali ya rufaa ya mkoa maweni iliyopo mkoani Kigoma.
  • Akikabidhiwa hospitali hiyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa anashukuru sekretarieti ya mkoa kwa kuisimamia hospitali hiyo pamoja na watumishi katika kipindi hicho na hivyo kuwezesha wananchi kupata huduma zinazostahili.
  • “Pamoja na makadhibiano tutaendelea kushirikiana kwa ukaribu na ofisi yako RAS na bado utaendelea kuwasimamia watumishi hawa kwani wapo mkoani kwako”.
1-01
Katibu Mkuu wizara ya afya Dkt. Zainab Chaula akisaini ripoti ya taarifa ya hospitali ya rufaa ya mkoa ya maweni,makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera
  • Aidha, Dkt. Chaula amesema wizara yake wametengeneza mkataba kati ya Wizara na RAS katika eneo la usimamizi hasa ya majengo ili yaweze kubaki kwenye uimara unaohitajika.
  • “Tunawashukuru watendaji wa ofisi ya katibu tawala kwa kazi nzuri waliyoifanya ya usimamizi wa hospitali hiyo hadi sasa tunakabidhiana, tutakwenda kuzisoma nyaraka hizi moja baada ya nyingine, maana ni mali za Serikali, mmetueleza kuna madeni tutayapitia na kuyafanyia kazi,” alisema.
  • Naye Katibu Tawala wa mkoa wa kigoma Rashid Machatta alisema kwamba bado ataendelea kushirikiana kwa ukaribu na watumishi wa hospitali hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao ili wananchi waweze kupata huduma bora
2-01
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta akisaini ripoti ya makabidhiano ya hospitali ya rufaa ya mkoa maweni, kushoto akishuhudiwa na Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula
  • “ Watumishi sisi bado ni wamoja, tutashirikiana bega kwa bega ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma zilizo bora”.Alisema Rashid Machatta.
  • Wakati huo huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Osmond Dyegula alisema hospitali hiyo ina jumla ya watumishi 233, kwa wastani wanaona wagonjwa kati ya 300 hadi 330 kwa siku kutokana na takwimu za mtuha za mwaka 2018/19.
  • Wizara ya afya imekabidhiwa hospitali hiyo ikiwa ni agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhamishia usimamizi huo wizara ya afya mwaka 2017 kutoka chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).Na. Catherine Sungura– Kigoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KALENGE WAKAMILIKA

Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani Uvinza wameishukuru kwa Serikali kukamilika ujenzi wa zahanati na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *