Afya BIMA YA AFYA Taarifa Vyombo vya Habari Taarifa ya Habari Tanzania MpyA+ WIZARA YA AFYA

SERIKALI YAPOKEA MSAADA KUKABILIANA NA CORONA (COVID-19)

  • Serikali imepokea msaada wa vifaa-tiba kutoka China kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya homa ya mapafu inayoambukizwa na kirusi mpya aina ya Corona (COVID-19), huku ikiishukuru kwa kushiriki kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huu.

IMG_1305

  • Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Muhammed Bakari Kambi amesema msaada huo ambao umetolewa na Taasisi ya Alibaba ya mfanyabiashara bilionea wa China Jack Ma ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliobainika kuwa na homa hiyo, vitendanishi (Rapid Tests) 20,000 na Barakoa (Masks) 100,000.

IMG_1308

  • Prof. Muhammed amesema msaada huo utawasaidia wataalamu wa afya nchini wakati wa kuwahudumia waliobainika na watakaobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

IMG_1307

  • “Tumekuja hapa kushuhudia sehemu ya shehena ya tani tatu ya vifaa-tiba vilivyotolewa na Taasisi ya Jack Ma na Alibaba ambavyo vimewasili usiku wa leo na ndege ya mizigo ya Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia Ethiopia,” amesema Prof. Muhammed.
  • Katika hatua nyingine, Prof. Muhammed amemshukuru Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia Ethiopia Ndg. Tewodros Girma ambaye amekabidhi msaada huo kwa niaba ya Balozi wa nchi hiyo, Mhe. Yonas Yosef. WAMJW – Dar es Salaam

IMG_1306

Matokeo ChanyA+
Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.
http://matokeochanya.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.