Afya BIMA YA AFYA MAZAO YA BIASHARA Taarifa Vyombo vya Habari Taarifa ya Habari Tanzania MpyA+ WIZARA YA AFYA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

SERIKALI YAWAKUTANISHA WAZALISHAJI WA MALIGHAFI ZINAZOTUMIKA KUTENGENEZA VITAKASA MIKONO (HAND SANITIZER).

IMG-20200325-WA0086
Baadhi ya washiriki wa kikao cha wadau wa sekta ya viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer)wakimsikiliza waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa,(hayupo pichani)
 • Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa Machi 25 amefanya kikao na wamiliki na wasimamizi wa Viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono ( Hand Sanitizer).
 • Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana na wenye viwanda, wazalishaji pamoja na wadau wengine watakavyoweza kuongeza uzalishaji ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa kwa ajiri ya kujikinga na usambaaji wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID19).
IMG-20200325-WA0088
Wadau wa sekta ya viwanda ambao ni wamiliki na wasimamizi wa viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono (Hand Sanitizer)walipokutana kwenye kikao na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa machi 25 jijini Dodoma.
 • Katika kikao hicho Kampuni la Kilombero Sugar imetoa lita 30,000 za alcohol bure kwa serikali zitaakazosaidia kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer) ili kusaidia juhudi za serikali za kupambana na virusi vinavyosababisha ugojwa wa Corona.
 • Pia kampuni ya Consumer Choice Ltd imetoa kwa serikali kiasi cha lita 10,000 za ethanol na pia imeamua kubadili matumizi ya Ethanol ambayo yalipaswa kutengeneza vilevi ambapo asilimia 75% za Ethanol zitatengeneza vitakasa mikono (hand sanitizer) na 25% ya Ethanol itakayobaki itatumika kutengeneza vilevi.
IMG-20200325-WA0089
Baadhi ya washiriki wa kikao cha wadau wa sekta ya viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono(Hand Sanitizer)wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa.
 • Kampuni ya Mount Meru Millers imetoa lita 10,000 ya Vitakasa mikono (Hand sanitizer) itakayosambazwa kwa vituo vya afya na taasisi nchini.
 • Waziri Bashungwa ambaye ni mbunge wa Karagwe amewataka wenye viwanda kuongeza uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vitakasa mikono pia amewaelekeza TBS na FCC kuendelea kukagua wafanyabiashara wa vitakasa mikono ambao wanauza bidhaa feki na hafifu pia kwa wote wanaopandisha bei kwa lengo la kujinufaisha kuwachukulia hatua kali za kisheria kwani wanahatarisha maisha ya watanzania.
IMG-20200325-WA0090
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akizungumza katika kikao na wamiliki na wasimamizi wa viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer)
Matokeo ChanyA+
Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.
http://matokeochanya.co.tz

One thought on “SERIKALI YAWAKUTANISHA WAZALISHAJI WA MALIGHAFI ZINAZOTUMIKA KUTENGENEZA VITAKASA MIKONO (HAND SANITIZER).

 1. ni jambo zuri sana kukutana na kujadiliana masuala muhimu ya Taifa letu.
  endelea kukutana na makundi mbalimbali yenye nafasi ya kusadia na kuchangia mapamban haya hatari kabisa.
  hongera sana KomredI Bashungwa

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.