Recent Posts

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ina Mchango Mkubwa katika Mipango na Sera za kuendeleza Uchumi wa Buluu unaozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi Jengo la Taaluma na Utawala la taasisi hiyo Buyu ,Wilaya ya Magharibi B ,Mkoa wa Mjini Magahribi. Aidha Rais Mwinyi ameahidi Serikali kuendelea Kushirikiana na Taasisi hiyo wakati wote kwa lengo la kuhakikisha Rasilimali za Bahari ziliyopo zinatumika ipasavyo ili kutoa Mchango …

Soma zaidi »

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga zaidi ya shilingi bilioni 250 katika mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi katika Halmashauri zote 184 nchini

Taarifa hii imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange, wakati akijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Chaya, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki. Dkt. Chaya alitaka kufahamu mpango wa Serikali wa kupeleka jokofu la kuhifadhia maiti katika Kituo cha …

Soma zaidi »

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiambatana na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameungana na Waumini mbalimbali katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu na Mwaka Mpya 2025 iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma

Akizungumza na waumini mara baada ya Misa hiyo, Makamu wa Rais ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali kuwatakia watanzania wote heri na baraka kwa mwaka mpya 2025. Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wa dini, …

Soma zaidi »