Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kuidumisha hali ya amani na utulivu ambayo ndio msingi wa mafanikio yanayoendelea kupatikana hivi sasa na yatakayopatikana hapo baadae. Dk. Shein aliyasema hayo leo katika risala yake ya kuukaribisha mwaka mpya wa …
Soma zaidi »Maktaba ya Mwaka: 2018
STEMPU ZA KIELEKTRONIKI ZA USHURU WA BIDHAA KUANZA KUTUMIKA JANUARI, 2019
Bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa kama vile sigara, mvinyo, pombe kali pamoja na bia zitaanza kutumia rasmi stempu za kielektroniki Januari, 2019 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na Mbeya ambapo mfumo wa stempu hizo umeshafungwa kwenye mitambo ya uzalishaji. Akizungumza mara baada ya kumaliza …
Soma zaidi »NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya Kome na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi …
Soma zaidi »WAZIRI KALEMANI AWATAKA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME KUELEZA MIPANGO KAZI YAO KWA VIONGOZI
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchini kote, kuwasilisha mipango-kazi yao kwa viongozi na wawakilishi wa wananchi wa maeneo wanakofanyia kazi ili waweze kuielewa hivyo kusimamia utekelezaji wake. Alitoa maagizo hayo jana, Desemba 30, 2018 wilayani Ukerewe akiwa katika ziara ya kazi kukagua …
Soma zaidi »SHILINGI BIL. 222 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO – WAZIRI MKUU MAJALIWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222 zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kuwataka wakulima wawe na subira. Amesema wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na uhakiki kisha …
Soma zaidi »WAZIRI MPANGO ATOA TAARIFA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI 2018/2019
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO HALI YA UCHUMI WA TAIFA NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI 30 Desemba 2018, Dar es salaam. Pato la Taifa (kwa bei za 2007) Uchumi wa Taifa umeendelea kuwa imara, ukikua kwa 7.1% (2017) ikilinganishwa na wastani wa ukuaji wa …
Soma zaidi »WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UENDELEZAJI MIJI YA KIMKAKATI KATIKA JIJI LA DODOMA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma na kukagua ujenzi wa maegesho ya malori makubwa katika eneo la Nala na uboreshwaji wa mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangalijijini Dodoma. Pia amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi andelee kutenga …
Soma zaidi »WAITARA AZITAKA HALMASHAURI ZOTE KUTEKELEZA MPANGO WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI NCHI NZIMA
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara amezitaka Halmashauri zote kutekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi nchi nzima kwenye Halmashauri zao bila ya kutumia kisingizio cha ukosefu wa bajeti za kufanya vikao vinavyohusu utoaji wa majina ya mitaa …
Soma zaidi »MKANDARASI JENGO LA WIZARA YA NISHATI ATAKIWA KUKAMILISHA KAZI YA UJENZI KWA WAKATI
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemtaka mkandarasi anayetekeleza kazi ya ujenzi wa Jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa. Akizungumza katika eneo la Ihumwa WaziriKalemani amesema kuwa, ili kufanikisha utekelezaji wa kazi hiyo kwa wakati …
Soma zaidi »