“Na kazi ya Awamu hii ya tano, ni kukamilisha mambo yote ambayo mwalimu alitamani yafanyike lakini alihujumiwa yasikamilike. Yepi hayo? Moja; Ni kuhamisha Makao Makuu kwenda Dodoma…”
“Nendeni msome hansadi za Registrative council mwaka 1959.. Waingereza wanazungumzia ..wakoloni wale..watawala wale.. kuhamishia makao kwenda dodoma. Shida ilikuwa ni fedha! Nendeni msome hansadi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za mwaka 69 (1969) msome maelezo ya kina ya Joseph Kizurira Nyerere mdogo wake wa Mwalimu ya kwanini tuhamie Dodoma. Na mwaka 72 (1972) maamuzi yalifanyika. Mwaka 74 (1974)CDA iliundwa..Wizara iliundwa na juhudi zilianza. Lakini baada ya hapo, vita vikaja (Vita ya Kagera)Na master plan ya Dodoma ilitengenezwa na kampuni ya Canada..na kampuni ya Ki-Australia.. Na nchi fulani ya kiafrika ilikuja kufanya study tour kujifunza..wao wakachukua Dodoma yoote wameijenga kwao! na nchi hiyo..kwa sababu mimi ni waziri siwezi kuitaja.Unajua tunafanya vitu.. halafu baada ya hapo tunajibeza wenyewe…”
“Lakini leo: Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.. na ambaye maamini yawezekana akawa ndiye Rais wa mwisho wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyemuona mwalimu akiwa na akili timamu yaani yeye mwenyewe akiwa ni mtu mzima; Watakaofuata kuongoza nchi yetu, mwalimu atakuwa ni hadithi ya mbali. Ndio maana Rais wetu.. sio tu ni mfuasi wa Mwalimu.. Sio tu ni muamini wa Mwalimu..; Lakini ameamua kumaliza miradi yote aliyoianzisha mwalimu…”
“..Ujenzi wa bwawa la Stieglers Gauge, ni ndito ya mwalimu uliamriwa mwaka 75 (1975)! Aliamua kujenga lile bwawa.. na akaenda mbali.. akaunda shirika la kusimamia maendeleo..RUBADA..Rufiji Basing Development Authority. Kwanini tulishindwa kujenga ule umeme..; Hatukuwa na fedha! Na wenye fedha Benki ya Dunia walisema Tanzania hamuhitaji umeme.. shida yenu ni MEGAWATTS 100. Tengenezeni Kidatu na Mtera inatosha. Leo hii Kidatu na Mtera inatosha? Na lugha hiyo hiyo inarudiwa sasa!; Ebo? Sisi ni wajinga? Once bitten twice shy. Kwani kuna dhambi gani kuwa na umeme ulio wa ziada? Umeme wote tulionao sasa Tanzania ni MEGAWATTS 1,460. Huu (kutoka Stieglers Gauge) utakuwa MEGAWATTS 2,100 na bado hautoshi…”
“..Shida ya leo sio fedha.. sasa imezuka shida nyingine.. ambayo selikali inaifanyia kazi; Mazingira.. Na mimi siyapuuzi mazingira kwa sababu sheria ya mazingira anafahamu ndugu yangu Wilson Masilingi; Mimi niliporudi nyumbani nilikuwa kwanza consultant.. lakini baadae nilipelekwa ofisi ya Makamu wa Rais..kutunga ile sheria na kanuni. Lakini eneo ambalo utajengwa ule mradi wa Steglas Gauge ni asilimia tatu tu (3%) la eneo lote la hifadhi ya Selou. Na eneo la Selou lina ukubwa wa Kilometa za mraba hamsini na tano elfu (55,000). Mkoa wa Tanga unaingia mara mbili.. Mkoa wa Dodoma ni mdogo!.. Na nchi fulani za jirani sizitaji. Zote mbili zichukue zinaingia kwenye Selou na inadaki! (Eneo kubwa la hifadhi ya Selou) Lakini haraka sana tumesahau. Hakuna nchi imeendelea bila umeme. Someni Glad Bill Leaning.. Na sisi wa zamani tulizoma kwenye Development Studies. Lkini ulikuwa mrani wa Mwalimu. Tumpongeze sana Rais Magufili kuamua kukamilisha hayo!….” – Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi, Waziri wa Sheria na Katiba
02. 09. 2018
Seattle, Marekani