MKUU WA WILAYA YA HAI ACHUKUA HATUA SHAMBA LA KIBO AND KIKAU ESTATE KUKWEPA KULIPA KODI YA SERIKALI MILI 700

MKUU wa wilaya ya Hai Mh. Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa na kuwekwa rumande kwa saa 48 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate Bwana Jensen Natal pamoja na Manasheria wa kampuni hiyo Bwana Edward Mroso.
 
mbali na kukamatwa kwa watu hao Mkuu huyo wa wilaya ameamuru kushikiliwa kwa muda kwa Pasi ya kusafiria ya anayetajwa kuwa mwekezaji wa Shamba la Kibo and Kikau Estate Bwana Trevor Robert kutokana na tuhuma za kukwepa kulipa kodi ya serikali inayokadiriwa kuwa Zaidi ya Sh Mil 700.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley ,Jensen Natal akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya kabla ya kuingia katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiangalia pasi ya kusafiria ya anayedaiwa kuwa mwekezaji wa katika shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Trevor Robert raia wa Zimbabwe ambalo anatajwa kutokuwa na uhalali wa kuwa mwekezaji wa shamba hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo walipotembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate linatajwa kuwa na mwekezaji asiye halali. 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akimsikiliza Meneja wa Shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Trevor Robert wakati akitoa maelezo ya uhalali wa kuwekeza katika shamba hilo.
Askari Polisi wakiwa wamemshikilia ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Tanzania,Jensen Natal inayotajwa kukwepa kulipa kodi ya serikali kutokana na uwekezaji katika shamba la Kibo and Kikafu Estate,Natal amekamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai.
Askari akimsindikiza Mwanasheria wa kampuni ya Tudeley Tanzania,Edward Mroso baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TudeleyTanzania,Jensen Natal na Mwanasheria wa kampuni hiyo,Edward Mroso wakiwa kwenye gari la Polisi muda mfupi baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo baada ya kutembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate.
 
 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazin.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA NA RAIS WA NIGER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *