Kiwanda: Mzee Mbanga amesema “kukutana na Waziri kumenipa nguvu ya kufungua kiwanda changu”

Mtanzania aliyeunda BAJAJI, Mzee Andrew Mbanga amesema anatarajia kufungua kiwanda cha kutengeneza chombo hicho kwa sababu amepata nguvu baada ya kukutana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage.

Mzee Mbanga amesema kukutana na Waziri kumempa nguvu ya kufungua kiwanda chake ambapo awali alishindwa kwa sababu BAJAJI aliyounda ilikosa kibali. “Amenipa nguvu na kufikiria nitengeneze kiwanda changu mwenyewe,” amesema.

Ad

Amesema kuwa wazo la kuunda BAJAJI alilipata kutokana na sera ya Rais John Magufuli kuhusu uchumi wa viwanda, ambapo akaona na yeye atafute jambo la kuunga mkono sera hiyo.

“Nilijiuliza nitamuunga vipi mkono Rais wangu, nikasema lazima nifanye jambo ambapo nikafikiria kuunda Bajaji itakayoweza kuwabeba watu 6 ili kurahisha usafiri na kujiongezea kipato,”amesema.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *