YANGA: Mashabiki wachangia zaidi ya Mil 20 kwa kipindi cha mwezi mmoja

Baada ya kuwepo kwa taarifa za kufungiwa na FIFA kwa kiungo wa Yanga Mohamed Issa Banka, kwenye kipindi hiki uongozi wa klabu hiyo kwa mara ya kwanza umetoa kauli.

Kwenye kipindi hiki, uongozi wa klabu ya Yanga umeanza kwa kutoa taarifa kuhusu michango iliyokwishatolewa hadi sasa kupitia kampeni maalam ya kuichangia klabu inayoendelea.

Kiasi kilichopatikana kwa mwezi Agosti mwaka huu kimewekwa hadharani Kaimu Katibu Mkuu wake Omary Kaaya. Naye Afisa Habari wa timu hiyo Dismas Ten amezungumzia sababu za Yanga kuahirisha mchezo wao wa kirafiki uliokuwa umepangwa kupigwa Septemba 5 mjini Kigoma dhidi ya Singida United.

Dismas Ten pia amezungumzia maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo wao wa Septemba 9 dhidi ya African Lyon ambao ni maalum kwaajili ya kulinda tembo. Kipindi hiki pia kinakuletea meneja mpya wa timu ya wanawake ya Yanga,

‘Yanga Princes’ ambaye ni Zameda Mageka pamoja na Kit Manager Salma Makweta. Mahojiano maalum na Nahodha wa Yanga Princes Frola Kayanda pia yanapatikana humu. Kama kawaida, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ ameendelea kufanya uchambuzi wa mwendendo wa timu dimbani, na safari anazungumzia jinsi timu hiyo ilivyoanza ligi msimu huu.

Kipindi hiki kimeruka Ijumaa na tarehe 07/09/2018.

Unaweza kuangalia pia

HARMONIZE NA VIKUNDI VYA UTAMADUNI VYANOGESHA SHEREHE ZA MIAKA 58 YA UHURU NA 57 YA JAMHURI UWANJA WA JAMHURI JIJINI MWANZA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.