DODOMA: Ujenzi wa stendi kubwa, MpyA ya Dodoma waanza.

• Ujenzi unagharimu Tsh. Bilioni 35.4

• Ujenzi unatarajiwa kuchukua miezi 15

Ad

• Stendi hiyo itakabidhiwa kwa serikali tayari kwa matumizi mwezi Septemba 2019

Bilioni 77 za Mradi wa Tscp zatekeleza Agizo Rais JPM Jijini Dodoma.

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Mradi wa Mpango Miji Mkakati ‘Tanzania Strategic Cities Project’ maarufu kama Tscp unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI umetekeleza Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa Fedha zaidi ya Tsh. Bil 77 kwa ajili ya kujenga miundombinu katika Jiji la Dodoma.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini miradi hiyo itakayotekelezwa kupitia mradi wa Tscp Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amesema mradi huu wa kimkakati umelenga kubadilisha kabisa muonekano wa Jiji la Dodoma kwa kutekeleza yale aliyoagiza Mhe.Rais alipotangaza kuipandisha hadhi iliyokuwa Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji.

“Jiji hili lazima liwe la tofauti, lenye hadhi ya Makao Makuuu ya Nchi na livutie kuliko majiji yote Tanzania, tutaweka miundombinu ambayo itabadilisha kabisa muonekano wa Jiji, itaongeza fursa za biashara na kuwapunguzia kabisa adha wananchi wetu katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyalalamikia. Tuna imani kupitia kazi itakayofanyika hapa mtu aliyeondoka Dodoma mwaka huu akirudi baada ya miaka miwili tutamshika mkono kumuelekeza mitaa ya Jiji la Dodoma, hapatakuwa kama palivyo sasa na mabadiliko yatayofanyika ni ya kimataifa” Alisema Jafo.

Kupitia hafla hiyo Mhe. Jafo aliwatahadharisha wakandarasi washauri wa mradi kusimamia mradi huo kwa mujibu wa taratibu na sheria na kuhahakisha thamani ya fedha inaonekana kwa kila kipengele kitakachotekelezwa.

“Mkandarasi mshauri wajibu wenu ni kuhakikisha kila kilichoainishwa kiinafanyika kwa wakati na kwa usahihi wakati huo huo kumshauri mteja wao ambaye ni Halmashuri kufanya yale yote yanayotakiwa ili kazi iende sawa na kumsimamia mkandarasi kufanya kazi hiyo kwa ubora wa hali ya juu na endapo utaenda kinyume na haya Wizara yangu haitasita kukuchukulia hatua kwa mujibu wa sharia” alisema Jafo.

Alimazia kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza miradi mikubwa mitatu kwa fedha za mkopo toka Benki ya Dunia yenye lengo la kuimarisha na kuboresha Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji pamoja na Mkoa mzima wa Dar es Salamm ili mamlaka hizo ziweze kukua kulingana mabadiliko tunayokwenda nayo kuelekea uchumi wa kati na ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi wake. Jafo alitaja miradi mikubwa ya miundombinu inayosimamiwa na Ofisi yake kuwa ni Mradi wa Mpango Miji Mkakati (Tscp) unatekelezwa kwenye Majiji na Manispaa 8 na Dodoma ikiwa ndani ya mradi huu ambao utagharimu jumla ya fedha za kitanzania sh Bil 840, Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(Dmdp) ambao ni maalumu kwa kushughulikia changamoto za Jiji la Dar es salaam nao utagharimu Tsh. Bil 660 pamoja na Mradi wa Uendelezaji na Uboreshaji wa Halmashauri za Miji(Ulgsp) unatekelezwa katika Miji 18 na unagharimu Tsh. Bil. 650.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa miradi ya miundombinu katika Jiji la Dodoma ameishukuru Serikali kwa kuleta Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi itakayofungua milango ya maendeleo katika Jiji la Dodoma.

Pia aliwakumbusha wananchi wa Dodoma kuitumia fursa hii ya upatikanaji wa miradi mikubwa kama chachu ya maendeleo ambayo itakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na kubadilisha maisha kutoka yalivyo sasa na kuwa bora zaidi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Bilinith Mahenge amesema miradi hii ni fedha nyingi sana na Serikali imeamua kuwekeza katika Jiji hili hivyo yeye kama msimamizi Mkuu wa shughuli za Mkoa huu atahakikisha atasimamia kwa karibu miradi hii ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu.

Akiwasilisha taarifa mradi Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi ametaja kazi zitakazofanyika kupitia mradi wa TSCP kuwa ni Ujenzi wa barabara za Lami Km 26.6, Taa za barabrani 913, mfereji mkubwa wa kusafirishia maji ya mvua Km 6.5, Ujenzi wa Stendi ya Kisasa, Soko kuu la Kisasa, vizimba 7 vya kukusanyia taka, kituo kikuu cha kuegeshea malori pamoja na bustani ya kupumzikia yenye viwanja mbalimbali vya michezo.

Aliongeza kuwa barabara za lami zitajengwa maeneo ya katikati ya mji, pembezoni pamoja na barabara moja kubwa ya mchepuko zitajengwa kwa kiwango cha Lami Ngumu (Concret Asphat) na zitakuwa na eneo la waenda kwa miguu, mifereji ya maji ya mvua pamoja na Taa za barabara zinazotumia nguvu ya jua.

Akizungumzai ujenzi wa stendi ya kisasa itakayojengwa eneo la Nzuguni Kunambi amesema itajengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa Ekari 87 itakua na uwezo wa kuegesha Mabasi Makubwa 250, Mabasi madogo na magari ndogo 600, Bajaji 300 na pia itakua na maeneo makubwa ya biashara pamoja na eneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) pamoja na mama lishe. Kazi hii  itachukua muda wa miezi 15 hadi kukamilika kwake.

1 (1).jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini miradi mikubwa ya uboreshaji wa miundombinu katika Jiji la Dodoma itakayogharimu zaidi ya Fedha za Kitanzania Tsh. Bil 77 pembeni  yake ni Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi.

dodoma MpyA.jpeg

#SisiNiTanzaniaMpyA+ ya #WachapaKazi Wazalendo wanaoleta Matokeo ChanyA+ 110% katika kujenga uchumi imara na madhubuti kwa Watanzania wote

Tazama video yenyewe

#MATAGA

Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *