Rais wa Tanzania amedhamiria na amejitoa mhanga kuijenga nchi ya Tanzania upyA+

DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI;

•Rais wa Watanzania wa Hali ya chini, Masikini, wenye shida, wahitaji, wenye kumudu mlo wa siku kwa taabu; akiwa na lengo la kuwainua, kuwapa nguvu ya Kufanya Kazi na kupata kipato,

Ad

• Rais mwenye kuwafanya watu wote wa nchi yake bila matabaka kuwa sehemu ya wanufaika wa uchumi wa Taifa,

• Rais mwenye lengo lenye hakika ya kweli ya kuwajumuisha Watanzania wote katika faida ya rasilimali na utajiri wa Taifa lao,

• Anayehakikisha Raia wa nchi yetu wanakaa meza moja ya haki na usawa kwenye huduma za kijamii BILA Rushwa, Kunyanyaswa, Kudharauliwa, Kubezwa, Kuzungushwa au hata kudhulumiwa, kuporwa ama kuibiwa..

• Kuwarudishia Watanzania hadhi halisi ya nchi yao; Nchi ya wawajibikaji.. ya wa Wazalendo, Wamoja ..wenye upendo, Utu, Ukarimu na Hofu ya Mungu

• Rais aliyeapa kuzikabili kero, shida, usumbufu, utata, njia tata na kuzitatua haraka kwa manufaa ya walio wengi; Watanzania wanyonge

• Rais aliyeshika Kitabu Kitakatifu na kula kiapo kupambana, kutokomeza na kukabili bila kuchoka matumizi mabaya ya fedha za Umma, Ufisadi, U-‘Mangi meza’, Uvivu, Uzembe, U-mimi, Upendeleo na Ulafi na Uhujumu Uchumi.

• Aliyedhamiria na kujitoa kuijenga nchi yetu upyA+, Tanzania mpyA+

• Rais anayeungwa mkono na sisi wote, Watanzania katika kuleta UKOMBOZI wa Kiuchumi kwa Taifa letu; maana #NiSisiSisi yaani #SisiNiTanzaniaMpyA+ inayopata Matokeo ChanyA+ 110% katika kila nyanja ya kukuza na kujenga Taifa thabiti, Taifa lenye uchumi imara na madhubuti unaonufaisha Watanzania wote

#MATAGA 💪🏿💪🏿

Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *