- Serikali imesema imejipanga vema kuhakikisha sekta ya nishati na hasa ya mafuta na gesi inawanufaisha Watanzania wote na kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta hiyo.
- Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano January Makamba wakati akifungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya mafuta na gesi wakati anamwakilisha mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
- Kongamano hilo limehudhuriwa na zaidi ya wadau 200 kutoka mataifa zaidi ya 75 duniani na moja ya ajenda ni kuangalia fursa ambazo zinaweza kupatikana katika sekta ya mafuta na gesi huku pia kongamano hilo likijita kuangalia fursa ambazo watanzania watanufaika nazo kutokana na uwepo wa miradi mikubwa inayoendelea nchini.
- Waziri Makamba amesema ujumbe wa Waziri Mkuu katika kongamano hilo ni kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta ya gesi na mafuta.
Baadhi ya washiriki wa kongamano wa mafuta na gesi wakisikiliza maada kuhusu sekta hiyo.
Waziri wa wizara ya Ardhi, nyumba, maji, nishati na mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.
Naibu waziri wa wizara ya nishati, Subira Mgalu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.