
Kufuatia uamuzi wa Mhe. Rais Magufuli kuwa Flyover ya makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela iitwe Mfugale Flyover, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema amesoma wasifu wa Mhandisi Patrick Aron Lipilima Mfugale na kueleza kuwa ameitumikia nchi akiwa Mhandisi kwa miaka 41 ambapo katika kipindi hicho ameongoza katika kubuni na kusimamia ujenzi wa barabara kilometa 36,258 zikiwemo kilometa 9,951 za lami na amebuni na kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa na madogo 1,400 yakiwemo madaraja makubwa ya Mkapa (Rufiji), Umoja (Ruvuma), Rusumo (Mara), Kikwete (Malagarasi), Nyerere (Kigamboni, Dar es Salaam), Magufuli (Kilombero) na Sibiti (Simiyu/Singida).

”Ndugu zangu; Nitoe wito kwa wataalamu hapa nchini. Waige mfano wa uchapakazi wa Mfugale (Eng. Patrick Mfugale) Mfugale hakupendelewa.. ni haki yake. Yako mengi aliyoyafanya kwa ajili ya nchi. Ametanguliza Utanzania badala ya kutanguliza ubinafsi” – Rais Magufuli, wakati akizindua daraja la juu la Mfugale katika makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam.

“Mwaka 2005.. Eng Mfugale alipewa tuzo na Mzee Mkapa kule Songea.. kama mfanyakazi bora. Alisimamia vizuri barabara za kule kusini, alisimamia ujenzi wa barabara ya Somanga – Matandu.. Nangurukuru..” – Rais Magufuli.

“Eng. Patrick Mfugale ni Mwenyekiti wa kikosi cha wataalamu wanaobuni na kujenga Dodoma Sports Complex ambayo iko kwenye usanifu sasa hivi.. Mbali na kuwa mtendaji Kuu waWakala wa Barabara nchini (TANROAD) ni mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) inayoendelea kujengwa..” -Mhandisi Prof. Ninatubu Lema

“Eng. Mfugale amekuwa mvumilivu na mwaminifu sana. Amekuwa mzalendo sana hata alipokandamizwa, alivumilia na kutulia.” – Rais Magufuli

Heko Eng. Patrick Mfugale kwa utumishi wako uliotukuka kwa Taifa.
kwani #SisiNiTanzaniaMpyA+ inayopata Matokeo ChanyA+ 110% inayojengwa na Watanzania wachapa kazi, wazalendo, waadilifu na waaminifu ili Taifa lifikie lengo la kuwa na uchumi imara na madhubiti kwa Watanzania wote.