ENG. MFUGALE NI MFANO WA KUIGWA KWA UTUMISHI ULIOTUKUKA TANZANIA!

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
LEO TAREHE 27 SEPTEMBA, 2018 AMEZINDUA DARAJA LA JUU LA MFUGALE TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM

Kufuatia uamuzi wa Mhe. Rais Magufuli kuwa Flyover ya makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela iitwe Mfugale Flyover, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema amesoma wasifu wa Mhandisi Patrick Aron Lipilima Mfugale na kueleza kuwa ameitumikia nchi akiwa Mhandisi kwa miaka 41 ambapo katika kipindi hicho ameongoza katika kubuni na kusimamia ujenzi wa barabara kilometa 36,258 zikiwemo kilometa 9,951 za lami na amebuni na kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa na madogo 1,400 yakiwemo madaraja makubwa ya Mkapa (Rufiji), Umoja (Ruvuma), Rusumo (Mara), Kikwete (Malagarasi), Nyerere (Kigamboni, Dar es Salaam), Magufuli (Kilombero) na Sibiti (Simiyu/Singida).

Ubunifu wa Eng. Mfugale
Daraja la Magufuli limebuniwa na Eng. Patrick Mfugale. Pia ujenzi wa daraja hili, umesimamiwa na Eng. Mfugale.

”Ndugu zangu; Nitoe wito kwa wataalamu hapa nchini. Waige mfano wa uchapakazi wa Mfugale (Eng. Patrick Mfugale) Mfugale hakupendelewa.. ni haki yake. Yako mengi aliyoyafanya kwa ajili ya nchi. Ametanguliza Utanzania badala ya kutanguliza ubinafsi” – Rais Magufuli, wakati akizindua daraja la juu la Mfugale katika makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam.

Ad
Ubunifu wa Eng. Mfugale
Daraja la Mkapa limebuniwa na Eng. Patrick Mfugale. Pia ujenzi wa daraja hili, umesimamiwa na Eng. Mfugale.

“Mwaka 2005.. Eng Mfugale alipewa tuzo na Mzee Mkapa kule Songea.. kama mfanyakazi bora. Alisimamia vizuri barabara za kule kusini, alisimamia ujenzi wa barabara ya Somanga – Matandu.. Nangurukuru..” – Rais Magufuli.

Daraja la Kikwete
Daraja la Kikwete limebuniwa na Eng. Patrick Mfugale. Pia ujenzi wa daraja hili, umesimamiwa na Eng. Mfugale.

“Eng. Patrick Mfugale ni Mwenyekiti wa kikosi cha wataalamu wanaobuni na kujenga Dodoma Sports Complex ambayo iko kwenye usanifu sasa hivi.. Mbali na kuwa mtendaji Kuu waWakala wa Barabara nchini (TANROAD) ni mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) inayoendelea kujengwa..” -Mhandisi Prof. Ninatubu Lema

Kazi  ya Ubunifu na Usimamizi wa Ujenzi ni Eng. Mfugale
Daraja la Umoja limebuniwa na Eng. Patrick Mfugale. Pia ujenzi wa daraja hili, umesimamiwa na Eng. Mfugale.

“Eng. Mfugale amekuwa mvumilivu na mwaminifu sana. Amekuwa mzalendo sana hata alipokandamizwa, alivumilia na kutulia.” – Rais Magufuli

Eng. Mfugale mbunifu na msimamizi wa ujenzi wote!
Daraja la Nyerere (Kigamboni) limebuniwa na Eng. Patrick Mfugale. Pia ujenzi wa daraja hili, umesimamiwa na Eng. Mfugale.

Heko Eng. Patrick Mfugale kwa utumishi wako uliotukuka kwa Taifa.

kwani #SisiNiTanzaniaMpyA+ inayopata Matokeo ChanyA+ 110% inayojengwa na Watanzania wachapa kazi, wazalendo, waadilifu na waaminifu ili Taifa lifikie lengo la kuwa na uchumi imara na madhubiti kwa Watanzania wote.

Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Oni moja

  1. Good speech God Bless our President Magufuli God Bless Tanzania

Leave a Reply to LILLIAN Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *