Mkoa wa Songwe, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupitia mpango wa kitaifa wa kudhibiti UKIMWI NACP Kwa kushirikiana na shirika la MHRP – HJRMRI wameandaa
huduma za upimaji wa afya zitakazo tolewa bure mkoani humo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa Bri. Jen Nicodemas Mwangela, amesema kuwa uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Nalyelye katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlowo, ambapo huduma zitakazotolewa ni upimaji wa VVU, presha (BP), kisukari, uzito na uchangiaji wa damu wa hiyari
Amesema kampeni hizo zinalenga kuhamasisha wananchi hususan wanaume kupima afya zao na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya siku ya uzinduzi jumamosi ya tarehe 29 september 2018.