Mkoa wa Songwe, kwa kushirikiana na  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupitia mpango wa kitaifa wa kudhibiti UKIMWI NACP Kwa kushirikiana na shirika la MHRP - HJRMRI wameandaa huduma za upimaji wa afya zitakazo tolewa bure.

MKOA WA SONGWE KUZINDUA KAMPENI ZA UPIMAJI AFYA BURE

Wadhamini na wadau wa Afya wanaoshirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuzindua na kuendesha kampeni ya upimaji Afya mkoani humo itakayofahamika kama Furaha Yangu

Mkoa wa Songwe, kwa kushirikiana na  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kupitia mpango wa kitaifa wa kudhibiti UKIMWI NACP Kwa kushirikiana na shirika la MHRP – HJRMRI wameandaa
huduma za upimaji wa afya zitakazo tolewa bure mkoani humo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa Bri. Jen Nicodemas Mwangela, amesema kuwa uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika  uwanja wa shule ya sekondari Nalyelye katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlowo, ambapo huduma zitakazotolewa  ni upimaji wa VVU, presha (BP), kisukari, uzito na uchangiaji wa damu wa hiyari
Amesema kampeni hizo zinalenga kuhamasisha wananchi hususan wanaume kupima afya zao na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya siku ya uzinduzi jumamosi ya  tarehe 29 september 2018.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KALENGE WAKAMILIKA

Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani Uvinza wameishukuru kwa Serikali kukamilika ujenzi wa zahanati na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *