“Mabenki yetu anzisheni utaratibu wa kuweka.. dhamana, kuweka madini ya wananchi.. nunueni dhahabu. Nunueni dhahabu; Ili hawa wananchi badala ya kuhangaika kwenda kwenye minada amabapo wanalaliwa laliwa, aende benki ahifadhi kule.” – Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa
“Badala ya kuleta fedha eweke madini yake.. atakuja kuyachukua mwakani nayo yatakuwa yameongezeka thamani. Kwahiyo nitoe wito kwa mabenki badilikeni! Pokeeni madini azisheni hicho kitengo cha kupokea madini dhahabu, wekeni..” – Mhe. Waziri Mkuu
“Kwahiyo Mkurugenzi Mkuu Benki Kuu; Pamoja na maelezo yote hayo, kaa na mabenki yako ya biashara.. kaeni anzisheni utaratibu wa kupokea dhahabu kwenye benki ili wachimbaji wadogo akichimba akipata gramu zake tatu – nne, akimbize benki kwenda kuweka pale kama fedha.. badala ya fedha anaweka madini yake. Siku ya siku akija, akiona bei nzuri.. anakuja anachukua hela kwa thamani hiyo.” – Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.