NFRA YARIDHISWA NA HALI YA UBORA WA NAFAKA

KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU WA NFA
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akikagua mahindi wakati wa ununuzi katika kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma

Zoezi la kununua nafaka ya mahindi kwa ajili ya akiba ya Taifa ya Chakula unaendelea katika maeneo mbalimbali kote nchini ambapo wakulima kwa kiasi kikubwa wameitikia wito umetolewa na Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi yasiyokuwa na ubora.

Pamoja na Ubora wa mahindi kuwa changamoto katika maeneo mengi nchini kutokana na hali ya msimu wa mwaka jana
kuwa na jua Kali na mvua za msimu jambo lilolopelekea Mazao kuharibika yakiwa shambani.

Ad
KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA TAIFA WA  HIFADHI YA CHAKULA
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.

Kwa upende wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa (NFRA) Bi.Vumilia L. Zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya ununuzi ambapo hivi tarehe 1 Oktoba 2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika kituo hicho.

Katika ziara hiyo ya Mtendaji Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma, Meneja wa Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya alieleza kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya kwanza ya ununuzi na hadi kufikia tarehe 1 Oktoba 2018 Kanda hiyo imeshanunua zaidi ya tani 6000.

AFISA UBORA WA NFRA
Afisa ubora wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Masanja akikagua mahindi kwenye kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.

Ili kuimarisha dhana ya Ushirika, Wakala umenunua kwa kiasi kikubwa mahindi kupitia vyama ya Ushirika na vikundi vya wakulima yaani SACCOS na AMCOS ambazo jumla yake zinakuwa 23 ambazo ndizo zilizobainishwa na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma.

Vumilia aonyesha kuridhishwa na hali ya ubora wa nafaka iliyonunuliwa na kuwahimiza watumishi wa NFRA kuendekea kusisitiza na kununua mahindi yenye vigezo vya ubora unaokubalika kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Chakula.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *