- Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.74.
- Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akipokea mashine hizo kwenye Bohari ya Dawa(MSD) jijini Dar.
- Waziri Ummy amesema kuwa Serikaki inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni lengo la kuhakikisha huduma za afya zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi.
- “Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali,hivyo tunaboresha na kuimarisha huduma za tiba na uchunguzi wa magonjwa katika hospitali zetu kuwa na vifaa vya kisasa zaidi na kuondokana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi”.Alisema,Waziri Ummy Mwalimu.
- Amesema mashine hizo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa 10 ambazo X-ray za zamani zimekwisha muda wake na zimekua zikiharibika mara kwa mara.
- Amezitaja hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi,Morogoro,Njombe,Ruvuma,
Simiyu na Singida pamoja na hospitali za Wilaya ya Magu na Nzega.
- Aidha,Waziri Ummy amesema katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Wizara yake imepanga kununua mashine za mionzi nyingine zipatazo ishirini na nne(24) zenye thamani ya shilingi bilioni 4.1 ambazo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za Mikoa na Wilaya ambazo hazina au zina X-ray za kizamani au chakavu.
- Akizungumza kwa niaba ya Waganga Wakuu wa hospitali zinazopelekwa mashine hizo,Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana Dkt.Mashack Shimwela alisema ujio wa mashine hizo za kisasa zitasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa uchunguzi za mionzi pia utunzaji wa mazingira tofauti na aina zilizokuwa zikitumika mwanzo
- Aidha,amesema mashine hizo zina ubora wa picha pia ina mifumo ya Tehama ambayo ni rahisi kusomwa hata nje ya hospitali husika endapo hakuna msoma picha
Ad