Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Seleiman.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Seleiman.
Prof. Kabudi yuko Zanzibar kwa ziara ya siku mbili na katika mazugumzo yao wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya Wizara zao katika mambo yote yanahohusu na yasiyohusu Muungano.
Mawaziri hao wamesisitiza umuhimu wa Wizara zao kuendeleza ushirikiano katika maeneo ya utungaji wa Sheria, kushirikiana kwenye mafunzo ya Mahakimu, waendesha mashtaka na waandishi wa Sheria.
Kwa pamoja wamekubaliana kukaa na kubainisha maeneo ambayo yanahitaji kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika.