Pamoja na uzinduzi huo, Mhe. Rukia ameendelea kuunga mkono wito wa serikali kwa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya kubangua korosho wilaya humo ili wakulima wanufaike zaidi na kuongeza thamani ya zao hilo sambamba ya ajira kwa wakulima na watakao ajiriwa katika viwanda vhivyo.
- Tarehe ya Uzinduzi 13/10/2018 siku ya Jumamosi
- Uzinduzi kufanyika MNERO NGONGO
- Utaanza saa tatu asubuhi (09:00 AM)
Sambamba na uzinduzi huo, kutakuwa na utaratibu wa mambo kadhaa ili kufanikisha uzaaji korosho bora na wenye tija kwa mkulima;
- Kutatolewa elimu ya mauzo ya korosho kwa mfumo wa Stakabadhi ghalani
- Mwongozo wa Mauzo ya korosho
- Kutatolewa elimu na maelekezo ya masuala ya kibenki.
- Viongozi wa serikali watakuwepo kwaajili ya kutoa maelekezo rasmi ya serikali kuhusu biashara ya korosho nchini.
- Wataalam wa afya watakuwepo ili kuongoza wakulima na wafanyabiashara wa korosho katika zoezi la upimaji afya kwa hiyari, kutoa elimu ya BIMA YA AFYA na uchangiaji wa damu.
- Kwa watakao fika muda uliotangazwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, kila mmoja atapewa T-Shirt moja bure.
- Michezo na burudani mbalimbali vitapamba uzinduzi huo.