MADINI: Waziri amaliza mgogoro wa wawekezaji Moro

Mgogoro uliodumu kwa miaka minane (8) baina ya wawekezaji wawili wa Budha na Zhong Fa katika eneo la Maseyu mkoani Morogoro ambalo ni la machimbo ya Marble umekwisha rasmi baada ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko kukutana na pande zote mbili katika eneo hilo.

Hatua hiyo iliyochukulia na Serikali ni baada ya kubainika kuwa kuna watu wa kati wanaonufaika na mgogoro huo kwa kujipatia fedha isivyo kihalali huku Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ikikosa mapato ya kodi ya huduma kutoka kwenye eneo hilo la uwekezaji.

Mbali na kubaini uwepo wa mgogoro huo kuwa unachochewa na watu wa kati, lakini pia amemtaka mwekezaji Zhong Fa kufuata sheria na taratibu za nchi kwa kulipia leseni kabla ya kuanza kazi ya kuchimba madini hayo.

Kutokana na mgogoro huo kupatiwa ufumbuzi Naibu Waziri Biteko amemtaka mwekezaji Zhong Fa kulipa malimbikizo ya kodi anazodaiwa ambapo mwekezaji huyo, Aston Ji Lee  amekubali kufanya hivyo na kwamba ataanza kufuatilia hatua hizo katika wizara husika.

Ad

Unaweza kuangalia pia

SOKO LA MDINI ULANGA LA KUSANYA MILIONI 396 NDANI YA MIEZI 5

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Ulanga wamenunua madini …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *