MO: Kailima awatoa hofu Watanzania

Naibu katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani awatoa hofu Watanzania kuwa nchi ipo salamaL licha ya kutokea kwa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Naibu katibu mkuu huyo amesema hayo mkoani Simiyu ambapo amesema tukio hilo haliwezi kuharibu sifa ya nchi nzima kwani matukio kama haya hutokea pia nchi nyingine duniani kote.

Ad

Katika hatua nyingine, Naibu katibu mkuu huyo amekabidhi nyumba 10 kwa Jeshi la Polisi mkoani Simiyu wilayani Maswa.

Nyumba hizo zilikuwa zikikaliwa na wakandarasi wa Barabara ya Maswa – Mwigumbi ambao wamekamilisha kazi zao.

Zaidi ya askari 33 wanatarajiwa kuishi ndani ya nyumba hizo, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati akiwa waziri wa Ujenzi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *