Miche milioni 60 ya miti mbalimbali ilipandwa katika mashamba huku miche milioni 30 ikitolewa wananchi na taasisi kwa ajili ya kupandwa
Kwa nini tunahitajika kupanda miti?
Tupande miti kwani maisha yetu yanategemea sana miti. Miti ni uhai.
Tunatakiwa kupanda miti na kuitunza ili ituletee faida.
Tupande miti ili tuokoe misitu yetu ya asili. Pia miti mingi inazuia mmomonyoko wa udongo na miti pia huzuia upepo mkali.
- Fahamu aina mbalimbali za miti.
Miti ya matunda / chakula: miembe, miparachichi, mikorosho,
michungwa, mifenesi na michenza.
Miti ya mbao: mininga, mikongo, mivule, grevilea, mikangazi, mipaini na
mikaratuzi.
Miti ya kuni / nishati: mijohoro, grevilea.
Miti ya kurutubisha ardhi: grevilea, mikesya, milusina.
Miti ya dawa: milonge, miarobaini.
Miti ya chakula cha mifugo: milusina.
Miti ya kuhifadhi maji: mikuyu, mikangazi.
Ad