Moja ya picha za gari lililotambuliwa na Jeshi la Polisi (baada ya uchunguzi wa kina kupitia kamera za CCTV za tukio la kutekwa kwa MO) likiwa limepigwa picha kwenye eneno ambalo mpaka sasa halijafahamika. Picha hii bado haijafahamika kama ilipigwa kabla au baada ya tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara MO Dewji.
Azungumzia hatua muhimu za oparesheni mbalimbali za jeshi la polisi kwa miezi mitano (Machi hadi Oktoba)
Oparesheni hiyo imeweza kukamata magari ya wizi 42 na yote yanaletwa Dar es Salaam kwaajili ya kuwarahisishia wananchi kwaajili ya utambuzi katika tarehe itakayotangazwa.
Hali kadhalika, silaha mbalimbali 190 na risasi nyingi zimekamatwa katika oparesheni hiyo ambapo wananchi raia wema walitoa taarifa kwa jeshi la polisi.
Ametoa taarifa kuwa udhibiti wa wahalifu unaendelea vizuri na baadhi ya wahalifu wamekamatwa katika mpaka wa nchi ya Msumbiji na Tanzania. Atoa rai kwa Watanzania kuacha kujishirikisha na uhalifu na badala yake kufanya shughuli za kimaendeleo.
IGP atoa taarifa ya kupotea kwa Bilionea mfanyabiashara Mohamed Dewji almaarufu kama MO kuwa jeshi la Polisi limeweza kutambua risasi mbili zenye ukubwa wa 9 mm zilizofyatuliwa wakati wa utekaji.
Hali kadhalika, Jeshi la Polisi limeweza kutambua gari lililotumika katika utekaji huo, kisha kubainisha aina ya gari, lililotokea nchi jirani ambapo imebainika kuwa liliingia nchini tarehe 01 Septemba, 2018 huku dereva aliyehusika kuliendesha ametambulika pamoja na mmiliki wa gari.
Aelezea namna CCTV kamera zilivyosaidia kubaini uelekeo wa gari hilo (Toyota Surf yenye namba AGX 404 MC
Fungua link hii kufuatilia mkutano mzima wa Afande Sirro na waandishi wa habari.