Moja ya picha za gari lililotambuliwa na Jeshi la Polisi (baada ya uchunguzi wa kina kupitia kamera za CCTV za tukio la kutekwa kwa MO) likiwa limepigwa picha kwenye eneno ambalo mpaka sasa halijafahamika. Picha hii bado haijafahamika kama ilipigwa kabla au baada ya tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara MO Dewji.

Late Live: IGP AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

KAMANDA WA JESHI LA POLISI, SIMON SIRRO
IGP Simon Sirro akiongea na waandishi wa habari leo kuwapa taarifa za utendaji na oparesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la Polisi nchini kwa kipindi cha miaze mitano iliyopita.
  • Azungumzia hatua muhimu za oparesheni mbalimbali za jeshi la polisi kwa miezi mitano (Machi hadi Oktoba)
  • Oparesheni hiyo imeweza kukamata magari ya wizi 42 na yote yanaletwa Dar es Salaam kwaajili ya kuwarahisishia wananchi kwaajili ya utambuzi katika tarehe itakayotangazwa.
  • Hali kadhalika, silaha mbalimbali 190 na risasi nyingi zimekamatwa katika oparesheni hiyo ambapo wananchi raia wema walitoa taarifa kwa jeshi la polisi.
  • Ametoa taarifa kuwa udhibiti wa wahalifu unaendelea vizuri na baadhi ya wahalifu wamekamatwa katika mpaka wa nchi ya Msumbiji na Tanzania. Atoa rai kwa Watanzania kuacha kujishirikisha na uhalifu na badala yake kufanya shughuli za kimaendeleo.
  • IGP atoa taarifa ya kupotea kwa Bilionea mfanyabiashara Mohamed Dewji almaarufu kama MO kuwa jeshi la Polisi limeweza kutambua risasi mbili zenye ukubwa wa 9 mm zilizofyatuliwa wakati wa utekaji.
KAMADA SIRRO
Kamanda wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Sirro akiwaonyesha waandishi wa habari picha ya gari linalosadikika lilitumika katika tukio la kuteka Mfanyabiashara Bilionea Kijana nchini Bwana Mohamed Dewji MO ambapo amewaomba wananchi watoe ushirikiano pindi watakapoliona gari hilo.
  • Hali kadhalika, Jeshi la Polisi limeweza kutambua gari lililotumika katika utekaji huo, kisha kubainisha aina ya  gari, lililotokea nchi jirani ambapo imebainika kuwa liliingia nchini tarehe 01 Septemba, 2018 huku dereva aliyehusika kuliendesha ametambulika pamoja na mmiliki wa gari.
PICHA YA GARI TOYOTA HILUX SURF
IGP Sirro akionyesha picha ya upande wa nyuma wa gari aina ya Toyota Hilux Surf lenye namba za usajiri za nje ya nchi AGX 404 MC ambalo katika kamera za CCTV (si picha hii) limeonekana ndilo lilitumika katika tukio la kumteka mfanyabiashara MO alipoenda kwenye mazoezi ya viungo COLOSSEUM HOTEL eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam siku ya alhamisji tarehe 11 Oktoba, 2018.
  • Aelezea namna CCTV kamera zilivyosaidia kubaini uelekeo wa gari hilo (Toyota Surf yenye namba AGX 404 MC

 

TOYOTA HILUX SURF AGX 404 MC
Moja ya picha za gari lililotambuliwa na Jeshi la Polisi kwamba ndilo lilitumika katika tukio la utekaji (baada ya uchunguzi wa kina kupitia kwa kina kamera za CCTV za tukio la kutekwa kwa MO) Pichani gari hili aina ya Toyota Hilux Surf likiwa limepigwa picha (si za CCTV) kwenye eneno ambalo mpaka sasa halijafahamika. Picha hii ambayo imepatikana katika jitihada za uchunguzi wa kitaalamu unaoendelea wa Jeshi la Polisi bado haijafahamika kama ilipigwa kabla au baada ya tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara MO Dewji.

Fungua link hii kufuatilia mkutano mzima wa Afande Sirro na waandishi wa habari.

Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI WA JESHI LA POLISI. MAGOGO – GEITA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *