- Ni ule wa kufutiwa kuchaguliwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2018/19 zaidi ya 680.
- Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Taaluma Prof. Bonaventure Rutinwa atoa ufafanuzi. Fuatilia katika video hii
- Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako atoa maelekezo kwa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuhakikisha wanafunzi wote 682 waliofutiwa kuchaguliwa kwao warejeshewe nafasi zao na tayari uongozi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam umewapa taarifa rasmi wanafunzi wote hadi usiku wa siku ya Jumatatu tarehe 22 Oktoba, 2018.
- Maamuzi ya kikao cha dharula baina ya Mhe. Waziri, UDSM na TCU ulikipa Chuo Kikuu UDSM kuongeza muda zaidi wa udahili. UDSM imeongeza wiki moja kwa wanafunzi wapya kutuma maombi yao ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwamba kila mwanafunzi awe na uhuru wa kuchagua chuo anachokipenda kusoma na suala la udahili lishughulikiwe na chuo husika. Tazama video ya maamuzi ya Prof. Nalichako katika link hii https://youtu.be/RAail7n-IqI
#SisiNiTanzaniaMpyA+
#MATAGA
Ad
Ad