Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akitoa zawadi kwa washindi wa shindano.

WANAFUNZI 12 WA VYUO VIKUU KWENDA MAURITIUS KUJIFUNZA ELIMU YA MASOKO YA MITAJI

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza katika utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la Masoko ya Mitaji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  • Wadau wamekuwa na mwamko katika sekta ya fedha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kisera kwa lengo la kuongeza uwelewa na kukuza uwekezaji kupitia masoko ya mitaji.
  • Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango ameyasema hayo wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu Masoko na Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya Mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama akitoa maelezo ya shindano hilo lililoratibiwa na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuwapata vijana mahiri wa masoko ya mitaji katika hafla ya utoaji zawadi uliofanyika jijini Dar es es Salaam.
  • Amesema kuwa masoko na mitaji kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji na uchumi kwa ujumla hapa nchini.
  • Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuendelea kuandaa shindano hilo katika kuwajengea vijana wa kitanzania kujiamini na kuweza kuwa wabobezi katika eneo hilo.
  • Amesema shindano hilo limeshirikisha wanafunzi zaidi ya 15000 sio kazi ndogo lakini ina manufaa kwa vijana wa kitanzania.
 Sehemu ya washiriki wa wanafunzi katika shiondano.
Sehemu ya washiriki wa wanafunzi katika shiondano.
  • Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama amesema kuwa washindi 12 kwa uwiano wa wasichana sita na wavulana sita waliopata alama za juu wamepata fedha sh.milioni 1.8 kwa kila mmoja na kupata safari mafunzo nchini Mauritius kujifunza mamlaka ya usimamizi wa Masoko ya Mitaji ya nchi hiyo, Soko la Hisa Mauritius na kampuni tano kubwa za utoaji wa huduma katika masoko ya mitaji.
  • Mkama amesema CMSA inaendelea kufanya jitihada za kuongeza idadi wataalam wa masoko na mitaji yenye lengo la kuanzisha na kuendeleza masoko ya mitaji , yenye ufanisi , uwazi na yenye kutoa haki sawa kwa washiriki wote.
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Dkt John Mduma
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Dkt John Mduma akitoa maelezo juu ya usimamizi wa bodi hiyo katika CMSA katika uandaji wa shindano hilo na mpaka kumalizika katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Oni moja

  1. Hongera sana watoto wetu,wanafunzi kwa hatua hii muhimu sana.
    Ningepewa nafasi pamoja nanyi ningechagua maafisa Biashara wachache nao washiriki sababu ni kada yenye umuhimu na.mchango mkubwa sana kwa Local Government na mtu mmoja mmoja nchini tatizo tumewasahau hata kilele zeo na maombi yao na utendaji kazi wao hakuna anae jali.
    Tunapoteza rasilimali hii muhimu kwa Taifa kwa maendeloeo ya viwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *