TANZANIA YAJIKITA KUFIKIA NCHI YA UCHUMI WA KATI KUPITIA TEHAMA

Naibu Katibuu Mkuu
Naibu Katibuu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi
  • Serikali imejikita katika kuhakikisha kuwa Sekta ya TEHAMA inakuwa chachu ya kufikia kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ili kutimiza malengo ya millennia ya maendeleo endelevu kabla ya mwaka 2030.
  • Hayo yamesemwa na Naibu Katibuu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi jijini Dubai unakofanyika Mkutano Mkuu wa Nchi wanachama wa Shitika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano duniani (International Telecommunication Union – ITU).
  • Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, Dkt. Yonazi amesema Serikali imejizatiti kuhakikisha kuwa, uchumi wa Tanzania unachangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta ta TEHAMA.
  • “Napenda kutumia nafasi hii kuiarifu dunia kupitia Mkutano huu maendeleo makubwa ya TEHAMA yanayofanyika nchini Tanzania kupitia kupitia Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Kufuatia uchaguzi wa mwaka 2015, Serikali iliyoko madarakani hivi sasa imetayarisha Sera Mpya ya TEHAMA inayoelekeza umuhimu wa TEHAMA katika kujenga uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania”, alisema Dkt. Yonazi.
  • Aidha, Dkt. Yonazi alisema Sekta ya TEHAMA imekuwa kwa kiwango kikubwa sana nchini na kubadilisha maisha ya Watanzania walio wengi vijijini na mijini pia. Aliongeza kuwa ushahidi wa maendeleo ya TEHAMA nchini unaonekana katika idadi ya watoa huduma za TEHAMA nchini, matumizi ya teknolojia mbalimbali, idadi ya watumiaji wa huduma mbalimbali zikiwamo za intaneti, simu na hata redio na runinga katika mifumo mbalimbali kupitia TEHAMA.
  • Alisema, katika kukuza matumizi ya TEHAMA, Tanzania imeamua kuruhusu teknolojia mbalimbali (technology neutrality) na kuwekeza katika kujenga mkongo wa taifa katika kuunganisha kila mkoa nchini. Kadhalika, mkongo huo umeunganishwa na nchi jirani zilizopakana na Tanzania. Pia alizungumzia kuhusu Tanzania kuwekeza katika kituo cha kutunza data cha kiwango cha kimataifa (Tier 3 data Centre).
  • Hali kadhalika Dkt Yonazi aliuambia Mkutano huo kuwa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Tanzania imeweza kuwa na watumiaji zaidi ya 41 milioni hadi kufikia juni 2018 ambayo ni sawa na kufikia 94% ya nchi nzima, huku wastani wa watumiaji wa intaneti ikifikia 45% kati ya watanzania wapatao milioni 55. Alisema nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyobaki yanafikiwa mwaka 2020.
  • Dkt. Yonazi alikumbushia Mkutano huo kuwa, Tanzania ilikuwa moja ya nchi za mwanzo kabisa kuingia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali na hivyo kuruhusu masafa katika bandi 700 yaliyokuwa yanatumikakatika mfumo wa analojia na sasa yanatumika katika mfumo wa intaneti wa mwendo kasi ili kuongeza chachu ya maendeleo ya uchumi wa Tanzania kupitia TEHAMA.
  • “Kufuatika maendeleo makubwa ya TEHAMA nchini, Tanzania inakaribisha wawekezaji katika sekta hii ili kuweza kushirikiana na sisi katika kuboresha TEHAMA na maendeleo ya wananchi wetu kwa ujumla” alisema DKt Yonazi alipokuwa nahitimisha hotuba yake.
  • Tanzania inashiriki katika Mkutano huu wa ‘ITU Plenipotentiary Conference’ unaofanyika mara moja kila baada ya miaka 4 ambapo chaguzi mbalimbali zitafanyika kuchagua viongozi wakuu wa ITU na nchi zitakazoingia katika Baraza la Utawala la ITU (ITU Council) ambapo Tanzania inagombea kuwa miongoni mwa nchi 13 za Afrika kuingia katika Baraza hilo. Katika uchaguzi uliofanyika leo Alhamisi tarehe 1 Novemba, Katibu Mkuu Houlin Zao na Naibu Katibu Mkuu Malcolm Johnson wamechaguliwa tna kuendelea na nyadhifa zao kwa miaka mingine minne.
Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *