Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika mkutano aliouhutubia kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto.

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE

MATAGA - 107-02
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.
  • Serikali imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya wakulima wa chai wa wilaya za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate uliosababisha kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kazi.
  • “Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilomo Prof. Siza Tumbo hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara moja.”
  • Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa leo (Alhamisi, Novemba 1, 2018) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto baada ya kutembelea kiwanda hicho .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
  • Waziri Mkuu amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai na kiwanda hicho  kwa ajili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi. Imeamua kukirudisha Serikali baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.
  • Kuhusu suala la madeni ya watumishi, ameagiza watafutwe na madai yaorodheshwe kwa ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la ajira ambazo zilipotea baada ya kiwanda kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali inataka kuona kiwanda kikifanya kazi.
  • “Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresh kilimo linafanikiwa na  wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake.”
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mponde wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo kukagua kiwanda cha chai cha mponde na kuzungumza na wananchi.
  • Amesema wakulima hao walikosea kwa kuunda Umoja wa Wakulima wa Chai (UTEGA) ambapo katika kusajili badala ya kuanzisha ushirika wao walisajili NGO ambayo ilikuwa na wanachama wake, huku kiwanda kikiwa kimeanzishwa kwa ajili ya wakulima wote, jambo ambalo lilisababisha mgogoro baina ya wakulima na viongozi wa UTEGA.
  • Waziri Mkuu ameongeza kuwa wakati mgogoro huo ukiendelea kati ya UTEGA na wakulima wa chai wasiokuwa wanachama wa NGO hiyo, uliibuka mgogoro mwingine baina ya wakulima wote pamoja na muwekezaji ambaye ni kampuni ya Mponde Tea Estate baada ya kukabidhiwa kiwanda hicho  na uongozi wa UTEGA bila ya wao kushirikishwa.
  • Amewasisitiza wakulima wafufue mashamba yao kiwanda ni cha  Serikali  hivyo watakuwa wamepata sehemu ya uhakikika ya kupeleka chai ambayo itachakatwa. Pia ameagiza Mrajisi wa Ushirika aende kwa wakulima na kutambua idadi yao pamoja na kujua                               ukubwa wa mashamba yao
WAZIRI MKUU JANUA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika mkutano aliouhutubia kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto.
  • Amesema baada ya kubaini idadi ya wakulima na ukubwa wa mashamba yao awasaidie katika kuunda vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kisha kuunda ushirikia wao ambao watautumia katika kusimamia zao lao la chai na kuhakikisha mkulima ananufaika.
  • Waziri Mkuu amesema zao la chai ni miongoni mwa mazao makuu sita ya kimkakati, mengine ni korosho, kahawa, tumbaku, pamba na chikichi, hivyo amewataka wafufue mashamba yao na waendelee kuiamini Serikali yao ambayo imejidhatiti kuwahudumia.
  • Awali,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makam wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba alisma Mgogoro huo wa kiwanda cha Mponde ulianza tangu mwaka 1999 na ilipofika mwezi Mei 2013, wananchi walimlalamikia kwa kushindwa kutatua tatizo hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.
  • Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli aliwaomba wananchi hao waendelee kuwa na subira wakati suala lao likiwa linaendelea kushughuliwa na Serikali. “Mgogoro huo umesababaisha kudhorota kwa uchumi kwa sababu wananchi wengi waliacha kulima chai baada ya kiwanda hicho kufungwa miaka mitano iliyopita.”
  • Hivyo Makamba ameiomba Serikali iwasaidie wakulima wa zao la chai kuwapa miche mipya pamoja na pembe jeo kwa ajili ya kufufua zao hilo na kukiwezesha kiwanda cha chai MPonde kupata malighafi kama ilivyokuwa hapo awali.
  • Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kuwa  tayari amekuja na wataalam kwa ajili ya kukagua mashine zote zilizopo kiwandani hapo ili mchakato wa kukiwasha uanze  mara moja.
  • Mwijage alisema “mimi kama Waziri mwenye dhamana ya viwanda nawaambia wananchi muondoe wasiwasi tayari kiwanda kimeshafunguliwa maana sitaondoka hapa Bumbuli mpaka kieleweke.”
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

58 Maoni

  1. In 2018, the basketball world witnessed one of the most remarkable transformations in NBA history. LeBron James https://los-angeles-lakers.lebronjames-ar.com one of the greatest players of our time, decided to leave his hometown Cleveland Cavaliers and join the Los Angeles Lakers.

  2. Maria Sharapova https://tennis.maria-sharapova-ar.com was born on April 19, 1987 in Nyagan, Russia. When Masha was 7 years old, her family moved to Florida, where she started playing tennis.

  3. Upcoming fantasy MOBA https://bladesofthevoid.com evolved by Web3. Gacha perks, AI and crafting in one swirling solution!

  4. Bella Hadid https://img-models.bella-hadid-ar.com is an American model who has emerged in recent years as one of the most influential figures in the world of fashion.

  5. Chelsea https://england.chelsea-ar.com is one of the most successful English football clubs of our time.

  6. Michael Jordan https://chicago-bulls.michael-jordan-ar.com is one of the greatest basketball players of all time, whose career with the Chicago Bulls is legendary.

  7. лучший дизайн интерьера https://dizayn-interera-doma.ru

  8. Muhammad Ali https://american-boxer.muhammad-ali-ar.com is perhaps one of the most famous and greatest athletes in the history of boxing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *