RAIS MSATAAFU JK ATUNUKIWA TUZO

  • Rais Mstaafu Kikwete Atunikiwa Tuzo Kwa Kuwapa Kipaumbele Wanawake katika Uongozi.

RAIS MSTAAFU JK

  • Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.
  • Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Namibia, Mheshimiwa Saara Kuugongelwa katika Mkutano wa 8 wa WAELE uliofanyika jijini Windhoek ambao ulijadili “Nafasi ya Mwanamke katika Amani na Maendeleo Endelevu Afrika”.

RAIS MSATAAFU JAKAYA AKIZUNGUMZA

  • Rais Mstaafu Kikwete ameishukuru WAELE kwa tuzo hiyo na kwa kutambua mchango wake katika kusukuma agenda ya ushiriki wa wanawake katika uongozi.
  • Amesema kuwa, hakufanya hivyo kwa kutegemea kupata tuzo siku moja, bali alitimiza wajibu wake wa uongozi wa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi za uongozi kwa kuwa ni haki yao na sio fadhila.
RAIS MSATAAFU JK AKIPOKEA TUZO
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipokea Tuzo ya Uongozi Uliotukuka kutoka kwa  Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.
  • Amewashukuru wanawake aliowateua kaika uongozi kwa kutomuangusha katika madaraka aliyowapa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

“KIPINDI CHA UCHAGUZI TUKIFANYA KAZI ZETU VIZURI NI KIPINDI CHA KUWAELEKEZA WATU”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *