RAIS MAGUFULI AKIKAGUA GWARIDE KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KULA KIAPO NOVEMBA 05, 2015.

RAIS MAGUFULI, MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Awamu ya Tano, imefanikiwa kubadili utendaji kazi wa serikali na kuwa wenye tija na kulinda maslahi ya Watanzania walio wengi (Wanyonge), kuanzisha vita dhidi ya wezi, majangili, mafisani na mikataba ya kinyonyaji ya madini na rasilimali za Taifa, kurudisha ari ya kujenga uchumi wa Taifa na kusimamia matumizi yenye ya fedha na mali za Umma, kupambana na vitendo vya kushwa sambamba na kubaini na kuondoa malipo yote hewa katika serikali (Mishahara, Ajira, Mikopo, Madeni, Miradi, Mikakati na bajeti.)    #SisiNiTanzaniaMpyA+

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SUHUHU HASSAN
Rais Magufuli kwa kushirikiana na wasaidizi wake wakuu (Makamu wa Rais na Waziri Mkuu) anatimiza nia yake ya kufanya mageuzi makubwa katika kujengaUCHUMI imara na madhubuti kwa Taifa na Watanzania wote huku akilinda na kutetea maslahi ya Watanzania walio wengi yaani wanyonge pamoja na kuweka utaratibu mpya wa uendeshaji wenye tija wa mashirika na taasisi za Umma (TTCL, ATCL, TRC, TPA, TANAPA, NIC, TRA, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Rufaa nchini na mengine ambapo ufanisi umeongezeka na Tanzania uchumi unakua). Hali kadhalika, amefanikiwa kuanzisha utaratibu wa Elimu Bure jwa wanafunzi wa Darasa la kwanza hadi kidato cha Nne, serikali kuhamia Dodoma, Ujenzi wa Miundombinu mbali mbali ikiwemo Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme kutoka Dar es Salaam hadi mikoa ya Magharibi mwa Tanzania, Ujenzi wa Flyover ya kwanza nchini eneo la TAZARA, uundwaji wa meli, ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege, bandari na ujenzi wa barabara za ghorofa katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujono eneo la Ubungo. #SisiNiTanzaniaMpyA+

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA MAJALIWA

Ad

Unaweza kuangalia pia

ATCL YAANDAA SAFARI MAALUM KWA WAFANYABIASHARA

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limeandaa safari kwa wafanyabiashara wazawa itakayofanyika Machi 4, 2020 kwenda …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *