WAZIRI MKUU AZINDUA MKAKATI NA MPANGO KAZI WA KUJUMUISHA MASUALA YA JINSIA NDANI YA BUNGE

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIKATA UTEPE
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Shughuli hiyo imeshudiwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai na mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.
SISI-NI-TANZANIA-MPYA---152
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kitabu cha Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge mara baada ya kuzindua Mkakati huo leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Anayefuata ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai, wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma wengine ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai, mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa (wa kwanza kushoto), wengine nyuma ni watendaji mbalimbali wa Mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP).
Ad

Unaweza kuangalia pia

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.