- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Kilimanjaro kufanya kazi kwa kushirikiana, kuheshimiana na kupendana.
- Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani humo.
- “Mheshimiane, muwajibike wote tunajenga Tanzania mmoja tutangulize maslahi ya Taifa na si maslahi binafsi” alisema Makamu wa Rais.
- Makamu wa Rais aliwasili mkoani Kilimanjaro tarehe 8 Novemba 2018 ambapo alifanya ziara katika Wilaya ya Rombo, Wilaya ya Moshi, Same, Mwanga, Siha na Hai.
- Katika ziara hiyo Makamu wa Rais alikagua miradi mbali mbali na kuweka mawe ya msingi katika ujenzi na mengine ufunguzi.
- Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais aliwataka Viongozi wa Halmashauri kukusanya mapato na kubuni njia zingine za kupata mapato, pia alizihimiza kufanya mambo yao ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria.
- Makamu wa Rais amezitaka halmashauri kutochukua ushuru wa mazao shambani na badala yake waanzishe soko maalum la mazao ambalo mkulima atapeleka mazao yake hapo.
- Aidha Makamu wa Rais alitoa maagizo kwa mkoa kuhakikisha wafanyakazi wa viwandani na msahambani wanapewa msaada wa kutambua na kupata haki zao za msingi.
- Kwa upande mwingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa mkoa wa Kilimanjaro una migogoro mingi ya ardhi ambayo hatua zitachukuliwa karibuni haswa kwa waliojimilikisha mashamba ya Ushirika na pia upo nyuma katika kulipa kodi za ardhi.
- Waziri wa Ardhi amesisitiza watu wote waliouziwa viwanja kwenye eneo la kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools wasiendeleze kwani hati zote 39 zimefutwa na eneo litakabidhiwa kwa Kituo cha Wawekezaji.
Ad