- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan amewataka wamiliki wa migodi na viwanda vya kuchenjua madini nchini kuzingatia haki na usalama wa wafanyakazi wao.
- Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachotengeneza madini ya Kinywe (Graphite), Mirerani Wilayani Simanjiro.
- Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Manyara.
- “Pamoja na kuwekeza kupata pesa na kutoa ajira, kulipa kodi ni muhimu kuzingatia afya ya mfanyakazi kwa kumlinda kwa kumpatia vifaa vya usalama kazini pamoja na haki zao” alisema Makamu wa Rais.
- Kiwanda cha Gomwanga Gem Ltd kinamilikiwa Mtanzania kwa asilimia 100%, kinazalisha tani 60 kwa siku na kimeajiri Watanzania 80 ambacho mpaka sasa kimezalisha tani 3730.
- Kwa upande mwingine Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairuki amesema kwa sasa Serikali imeweka zuio la kusafirisha madini ghafi mpaka yaongwezewe thamani hivyo amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia maelekezo ya Serikali.
Ad