SERIKALI IMEJENGA MAZINGIRA YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MAPINDUZI YA VIWANDA – MGOYI

  • Serikali imejenga mazingira kwa vijana kupitia mapinduzi ya viwanda  kwa  serikali ya awamu ya Tano chini Rais Dkt John Pombe Magufuli ambapo ndio suluhisho ya vijana wenye ujuzi kutumika katika viwanda hivyo.
  •  Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi katika mahafali ya 21 ya Chuo VETA Mikumi , amesema kuwa mafunzo  ya VETA  ndio uwanja mpana katika soko la ajira kwa vijana kujiajiri au kuajiriwa.
  • Amesema vijana waliohitimu ni zaidi 315 ambapo wanaenda katika soko la ajira hivyo wanaweza kujiunga katika vikundi na kuanza kuzalisha kile walichokipata kwa miaka waliosoma chuoni hapo.
Mchoro wa Ramani
Mchoro wa Ramani waliochora wanafunzi wa kozi ya ujenzi katika Chuo cha VETA Mikumi.
  •  Wanachuo 315 wamehitimu mafunzo kwa ngazi ya (Level) II na III, kati yao wavulana walikuwa 209 na wasichana 106.
  •  Amesema vijana hao wanahitaji mazoezi ya kutosha ili kuweza kupambana na soko la ufundi katika Jumuia ya Afrika Mashariki hivyo ili waweze kuwa na vigezo hivyo walimu wanahitaji kuongeza nguvu za ziada kwa vijana hao hasa walioko  bado katika masomo.
  •  Mgoyi aliwaasa vijana kutokuitegemea sana serikali katika kuwatafutia ajira  na badala yake watumie fursa ya mafunzo walio pata VETA Kwenda kutengeneza kampuni na kujiajiri wenyewe na kuajiri wenzao.
Aliyekuwa Mkuu wa Chuo
Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Christopher Ayo akitoa salam kwa wahitimu ambao alikuwa nao wakati akihudumu cheo hicho katika chuo katika mahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
  • Aliwaasa vijana kutokuwa waoga katika katika kazi zao kwa yale walio fundishwa na kuwa wajasili ili waweze kuwaambia wateje na kuwaaminisha wateja ya kuwa wao ni bora, kwani wateja hawawezi kuwaamini kama wao watashindwa kuwaaminisha.
  •  Mkuu wa Wilaya huyo ameiomba VETA kuchangamkia   fursa za uzalishaji  mali kama wanavyofanya Jeshi ni katika ujenzi wa uchumi wa viwanda
  • “VETA hatuna sababu ya kubaki nyuma kwa sababu wataalamu tunao na wanafunzi tunao wafundisha hawana tofauti yoyote na wale walioko katika secta zingine za uzalishaji”amesema Mgoyi
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki wa VETA Geofrey Sabuni akizungumza kuhusiana na mikakati ya VETA katika utoaji ujuzi kwa vijana katika kmahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
  • Nae Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo amesema Chuo cha VETA Mikumi na Shirika la Plan International.  Kwa mara nyingine tena, Chuo kiliingia mkataba na Shirika la Plan International kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana 1651 ikiwa wavulana ni 741 na wasichana ni 910, Stadi kwa vijana walemavu 80 kati ya hawa wavulana ni 45 na wasichana ni 35 katika vijiji vilivyopo Mikumi .
  • Amesema kozi walizozitoa kwa vijana wa vijiji mbalimbali kwa wenye mahitaji maalumu ni Umeme wa Majumbani, Ufundi Magari na Pikipiki, Udereva, Upishi na Mapambo, Uchomeleaji Vyuma, Ufundi Simu, Ushonaji, Useremala, Aluminium na Ujenzi wa Nyumba.
  • Munuo amesema  mradi huo uliamza kutoa mafunzo mwezi Oktoba, 2015 na kulimaliza kutoa mafunzo hayo mwezi Juni, 2018 kwa kuendesha kwa  mfumo wa mafunzo nje ya Chuo (outreach) na uanagenzi ili kusaidia jamii na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wenye ulemavu.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KILA MTANZANIA ANAWEZA KUWEKEZA, TUMIENI FURSA ZILIZOPO – WAZIRI KAIRUKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *