- Zaidi ya billioni 22 za Kitanzania zimetengwa kwaajili ya hatua ya kwanza ya ujenzi wa Kiwanda cha uundaji wa magari cha Youngsan Glonet Corporation (KOTA) kutoka Jamhuri ya watu wa Korea.
- Kiwanda hicho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya hatua ya awali ya kutiliana saini ya makubaliano ya ubia kati ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Automobile Limited, Dkt. Reginald Mengi na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Thomas Choi .
- Kati ya Septemba na Oktoba mwaka 2019, Tanzania itaanza kutumia gari la kwanza litakaloundwa hapa nchini.
Ad