NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA VIJANA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA TONY ELUMELU FOUNDATION(TEF)

NAIBU WAZIRI AKIZUNGUMZA

  • Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka Vijana wa Tanzania wenye mawazo ya kibiashara kuchangamkia fursa ya mtaji mbegu(seed capital) kupitia Taasisi ya Tony Elumelu Foundation (TEF) ambayo inatoa fursa ya Mtaji wa biashara kwa Vijana wa nchi 20 za Afrika.

MAVUNDE AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA

  • Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo katika Hotel ya Serena,Dar er salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi fedha kiasi cha Shilingi Bilioni moja na milioni mia moja (1,100,000,000) kwa vijana wa 48 kama Mtaji wa biashara ambapo kila mmoja atapa dola za kimarekani 10,000.
  • Fedha hizo hutolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya UBA Ndg Tony Elumelu kila mwaka kwa Wajasiariamali Vijana wa Afrika.

NAIBU WAZIRI AKIKABIDHI CHETI

  • Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA Tanzania Ndg Usman Isiaka amesema dhamira ya Taasisi hiyo ni kuwaandaa Vijana wa Afrika kutatua changamoto zinazowakabili pasipo kutegemea Serikali au misaada kutoka nje ya Bara la Afrika na kuwaendeleza ili kukua na kumiliki makampuni makubwa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI SHONZA: WAZAZI NDIYO WALEZI WA KWANZA WA MTOTO

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wazazi na familia kuwa …

Oni moja

  1. Ili kupata iyo fursa ya kibishara vigezo gani unatakiwa kuwa navyo?
    Mimi tayari nimesajili company na ninayo tin number kinachonisumbua Ni mtaji ya shili million 100,000,000 , kwa ajili ya kununua mashine ya na ujenzi wa factory biashara ninayotaka kuifanya Ni unga wa sembe ,na unga wa muhogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *