TANZANIA YASHINDA TUZO YA UTALII NCHINI URUSI

 

  • Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii duniani nchini Urusi kwa mwaka 2018 (The Best Destination to the World in the Category of Exotic Destination 2018).
  • Balozi wa Tanzania nchini Urusi Mhe. Maj. Gen. (Mst). Simon Mumwi atapokea Tuzo hiyo kutoka Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine” jijini Moscow kwa niaba ya nchi.

WATALII

  • Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “National Geographic Magazine” lililoshirikisha wapiga kura 263,000 kwa njia ya mtandao.
  • Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka saba tokea mwaka 2011, raia wa Urusi kupitia jarida hilo wanaichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii. Mwaka 2011, Zanzibar ilipata tuzo ya ‘Star Travel’ kama eneo bora zaidi la utalii wa ufukweni katika bara la Afrika na mwaka jana, Tanzania ilipata tuzo ya NGT na Tanzania ilishinda nafasi ya pili katika tuzo hiyo  katika kundi la eneo bora la utalii duniani.
  • “National Geographic Traveller Awards” (NGT Awards) ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii nchini Urusi na hutolewa na Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine”.

UTALII

  • Mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wetu Urusi, Wizara za Utalii za Tanzania Bara na Zanzibar, na Taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.
  • Kupitia juhudi hizi, idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kutoka Urusi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, idadi hiyo imeongezeka kutoka watalii 4,021 mwaka 2012 hadi watalii 10,060 mwaka 2017.
  • Wizara kupitia Ubalozi wetu itaendelea kuongeza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na tunategemea kwa kushirikiana na wadau wengine katika juhudi hizi, idadi ya watalii kutoka Urusi wanaokuja nchini itaongezeka zaidi.

 

Taarifa imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Ad

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

WATALII 450 KUTOKA ISRAEL WAKO NCHNI KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII

Watalii zaidi ya 450 kutoka Israel wamewasili nchini mwezi Desemba 2019 kwa ajili ya tembelea …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.