Vijana wa Nchi Jumuiya za Afrika Mashariki wametakiwa kumuenzi Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuishi maono yake na falsafa zake katika kujiletea maendeleo ya kijamii,kisiasa na kiuchumi kwasababu Mwalimu Nyerere aliamini katika ujenzi na ustawi wa Taifa kupitia Vijana na alihamasisha mara zote Vijana kuishi katika uzalendo na uadilifu mkubwa.
Hayo yamesemwa katika Hotel ya Golden Tulip na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu,wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Viongozi wa Vilabu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulikuwa unaongozwa na Kauli mbiu “Uhai wa Maono ya Mwl.Julius K. Nyerere kwenye kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki”.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mwenyekiti Mtendaji wa Vilabu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki Ndg. Gwakisa Makaranga amewataka Vijana wa Afrika Mashariki kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi na kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za kisiasa ili kuwa sehemu ya maamuzi kwa mustakabali wa maendeleo ya Vijana.
Mkutano huo wa siku moja ulijumuisha wabunge wa Bunge la EAC na Vijana wa Nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi.