- Wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wameswa na serilali kuvilinda na kuvitunza kwa kuacha kufanya shughuli za kijamii. kwenye maeneo hayo.
- Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo wakati wa ziara yake katika mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu.
- Akizungumza baada ya kukamilisha ziara yake kwenye mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Kalobelo amesema wananchi wanatakiwa kuvitunza vyanzo vya maji ili maji yaendelee kuwepo kwa matumizi ya kila siku.
- Amesema, chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni mto Ruvu, kukiwa na Ruvu juu na Ruvu chini na wananchi wanazidi kuongezeka karibia na mto huo.
- “Wananchi wanazidi kuongezeka kwenye maeneo ya vyanzo vya maji ikiwemo Mto Ruvu ambao ndio chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na katikka sheria za mazingira inawataka wananchi wakae mita 60 kutoka kwenye mto,”amesema Mhandisi Kalobelo.
- Ameeleza kuwa, wananchi wanaoishi kando ya maeneo hayo wanatakiwa kuacha kupanda miti inayonyonya maji au kutumia maji mengi bali wanatakiwa kupanda miti inayovutia maji kuwepo kwenye vyanzo hivyo.
- Mbali na hilo, Mhandisi amesema shughuli za kijamii ikiwemo kilimo na ufugaji vinaweza kusababisha kuharibu vyanzo vya maji na kusababisha kukosekana kwa maji ambapo kwa sasa maji yapo kwenye wastani unaowatosheleza wananchi wa Dar es Salaam kwa asilimia kubwa.
- Aidha, katika ziara hito, Naibu Katibu Mkuu aliambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja na Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mjumbe wa bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
- Mhandisi Kalobelo ametemebelea maeneo mbalimbali ya miradi ya ujenzi wa matenki na upanuzi wa mtambo utakaofanikisha kupatikana kwa maji kwenye maeneo yalioyokuwa hayapo kwenye mtandao hapo awali.
- Amewapongeza DAWASA kwa jitihada wanazozionyesha kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji na ametoa rai kwa wananchi wajiunge kwenye mradi huu ili wapate maji safi na salama.
Ad