Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA RAIS KENYATTA WAFUNGUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI NAMANGA
Kituo hicho ni miongoni mwa vituo 15 vya OSBP vinavyojengwa katika mipaka ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kurahisisha ufanyaji wa biashara miongoni mwa nchi hizo, kuharakisha huduma za mpakani, kuongeza mapato na kuimarisha usalama.
Ujenzi wa kituo cha Namanga OSBP umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali za Tanzania na Kenya ambapo miundombinu ya upande wa Tanzania imegharimu shilingi Bilioni 22.365.
Tangu kianze kutoa huduma kituo hicho kimesaidia kupunguza muda unaotumiwa kukamilisha huduma za mpakani (clearance) kutoa saa 1 hadi dakika 15, na pia upande wa Tanzania ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka shilingi Bilioni 41 hadi kufikia shilingi Bilioni 58 zinazotarajiwa mwaka huu.
Wakizungumza baada ya kuzindua kituo hicho Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Kenyatta wamewashukuru wafadhili wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho (AfDB na JICA) na wametoa wito kwa Watanzania na Wakenya kuongeza biashara kupitia mpaka huo, huku wakitaka wafanyabiashara wadogo wasibughudhiwe.
“Kenya ni ya 3 kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa uwekezaji Tanzania kwa hiyo Wafanyabiashara wa Kenya wanapopita hapa msiwaone kuwa ni maadui, halikadhalika Tanzania ni yenye mifugo mingi hasa ng’ombe kwa hiyo Watanzania wanapopeleka nyama Kenya nao wasikwamishwe” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
“Sisi tujione wana Afrika Mashariki, tuzilete nchi zetu pamoja na tuutumie umoja wetu wa watu takribani Milioni 200 kufanya biashara na kunufaika, hapa mpakani sisi viongozi tupatumie kurahisisha biashara na nyie wananchi muwe huru kufanya kazi zenu ilimradi msivunje sheria na kufanya biashara haramu” amesema Mhe. Rais Kenyatta.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameahidi kushughulikia tatizo la maji katika eneo la Namanga kwa kuwapelekea maji ya kutoka Longido ambako Serikali imejenga mradi mkubwa wa maji uliogharimu shilingi Bilioni 15.
Pia Mhe. Rais Magufuli ameishukuru AfDB baada ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Gabriel Negatu kueleza kuwa imeridhia kutoka fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Malindi – Lungalunga – Tanga – Pangani – Bagamoyo inayounganisha Tanzania na Kenya, na mradi wa barabara ya Rumonge – Manyovu – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi inayounganisha Tanzania na Burundi.
Baada ya kuagana na Mhe. Rais Kenyatta ambaye amerejea nchini kwake, Mhe. Rais Magufuli akiwa njiani kwenda Arusha Mjini amekutana na wananchi wa Odonyosamba wilayani Arumeru na kuahidi kushughulikia tatizo la maji linalolikabili eneo hilo ambapo ameagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa kusafisha maji kiasi cha shilingi Milioni 500 zitolewe wiki ijayo na pia amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa kufika katika eneo hilo ili kuangalia namna ya kufikisha maji ya kutoka mradi mkubwa wa maji Arusha Mjini kwa wananchi hao.
Mhe. Rais Magufuli pia amekutana na wananchi wa Mianzini katika Jiji la Arusha ambapo amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha Jiji la Arusha ikiwemo kujenga barabara za kisasa ndani ya Jiji hilo, kuwajali wafanyabiashara wadogo na kwamba kesho ataweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Arusha Mjini utakaogharimu shilingi Bilioni 520.
Hello there, just became aware of your blog through Google,
and found that it is really informative. I’m going to watch out for brussels.
I will be grateful if you continue this in future.
Lots of people will be benefited from your writing.
Cheers! Najlepsze escape roomy
I like this website it’s a master piece! Glad I found this on google.!