Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA RAIS KENYATTA WAFUNGUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI NAMANGA

MAGU-NA-UHURU-11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 01 Desemba, 2018 wamezindua kituo cha huduma kwa pamoja mpakani (Ones Stop Border Post – OSBP) katika eneo la Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya. Pamoja na kuzindua ofisi za kituo hicho katika pande zote mbili, Waheshimiwa Marais wamepanda miti ya kumbukumbu na kukagua utoaji wa huduma zikiwemo za forodha na uhamiaji.
MAGU-NA-UHURU-10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwa wameshikana mkono wakati wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
  • Kituo hicho ni miongoni mwa vituo 15 vya OSBP vinavyojengwa katika mipaka ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kurahisisha ufanyaji wa biashara miongoni mwa nchi hizo, kuharakisha huduma za mpakani, kuongeza mapato na kuimarisha usalama.
  • Ujenzi wa kituo cha Namanga OSBP umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali za Tanzania na Kenya ambapo miundombinu ya upande wa Tanzania imegharimu shilingi Bilioni 22.365.
MAGU-NA-UHURU-9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
  • Tangu kianze kutoa huduma kituo hicho kimesaidia kupunguza muda unaotumiwa kukamilisha huduma za mpakani (clearance) kutoa saa 1 hadi dakika 15, na pia upande wa Tanzania ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka shilingi Bilioni 41 hadi kufikia shilingi Bilioni 58 zinazotarajiwa mwaka huu.
  • Wakizungumza baada ya kuzindua kituo hicho Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Kenyatta wamewashukuru wafadhili wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho (AfDB na JICA) na wametoa wito kwa Watanzania na Wakenya kuongeza biashara kupitia mpaka huo, huku wakitaka wafanyabiashara wadogo wasibughudhiwe.
MAGU-NA-UHURU-8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
  • “Kenya ni ya 3 kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa uwekezaji Tanzania kwa hiyo Wafanyabiashara wa Kenya wanapopita hapa msiwaone kuwa ni maadui, halikadhalika Tanzania ni yenye mifugo mingi hasa ng’ombe kwa hiyo Watanzania wanapopeleka nyama Kenya nao wasikwamishwe” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
  • “Sisi tujione wana Afrika Mashariki, tuzilete nchi zetu pamoja na tuutumie umoja wetu wa watu takribani Milioni 200 kufanya biashara na kunufaika, hapa mpakani sisi viongozi tupatumie kurahisisha biashara na nyie wananchi muwe huru kufanya kazi zenu ilimradi msivunje sheria na kufanya biashara haramu” amesema Mhe. Rais Kenyatta.
MAGU-NA-UHURU-7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipanda mti mara baada ya mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
  • Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameahidi kushughulikia tatizo la maji katika eneo la Namanga kwa kuwapelekea maji ya kutoka Longido ambako Serikali imejenga mradi mkubwa wa maji uliogharimu shilingi Bilioni 15.
  • Pia Mhe. Rais Magufuli ameishukuru AfDB baada ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Gabriel Negatu kueleza kuwa imeridhia kutoka fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Malindi – Lungalunga – Tanga – Pangani – Bagamoyo inayounganisha Tanzania na Kenya, na mradi wa barabara ya Rumonge – Manyovu – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi inayounganisha Tanzania na Burundi.
MAGU-NA-UHURU-6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipata maelezo ya kituo hicho cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
  • Baada ya kuagana na Mhe. Rais Kenyatta ambaye amerejea nchini kwake, Mhe. Rais Magufuli akiwa njiani kwenda Arusha Mjini amekutana na wananchi wa Odonyosamba wilayani Arumeru na kuahidi kushughulikia tatizo la maji linalolikabili eneo hilo ambapo ameagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa kusafisha maji kiasi cha shilingi Milioni 500 zitolewe wiki ijayo na pia amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa kufika katika eneo hilo ili kuangalia namna ya kufikisha maji ya kutoka mradi mkubwa wa maji Arusha Mjini kwa wananchi hao.
MAGU-NA-UHURU-4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
  • Mhe. Rais Magufuli pia amekutana na wananchi wa Mianzini katika Jiji la Arusha ambapo amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha Jiji la Arusha ikiwemo kujenga barabara za kisasa ndani ya Jiji hilo, kuwajali wafanyabiashara wadogo na kwamba kesho ataweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Arusha Mjini utakaogharimu shilingi Bilioni 520.
MAGU-NA-UHURU-3
Baadhi ya Wananchi wa Kenya na Tanzania waliohudhuria katika hafla ya ufunguzi wa Vituo hivyo Mpakani Namanga.
MAGU-NA-UHURU-2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea upande wa mpaka wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa kituo cha kutoa huduma kwa pamoja kwa upande wa Kenya.

MAGU-NA-UHURU-1

MAGU-NA-UHURU-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea kupanda gari moja kutoka Arusha mjini kuelekea Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya.
MAGU-NA-UHURU-12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na watoto wawili kutoka Kenya waliofika kumpokea katika kituo cha kutoa huduma kwa pamoja kwa upande wa Kenya.
MAGU-NA-UHURU-13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea funguo kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
MAGU-NA-UHURU-14
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi funguo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *