- Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mfumo wa rada ya kuongozea ndege nchini unaojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
- Akizungumza na wanahabari waliofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo, Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa amesema ujenzi wa jengo hilo umekamilika na ufungaji wa vifaa unaendelea hivyo ifikapo Desema 21 wataweza kufanya majaribio.
- “Kama mnavyoona wanahabari kila kitu kimeshafanyika tunachomalizia ni mitambo midogo midogo inayotarajia kukamilika ifikapo wiki ijayo na tufanye majaribio ili kuona ni wapi pa kurekebisha au tuongeze kitu gani?,” amesema Mwakisasa.
- Nae mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye amesema mara baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, mfumo huo utaimarisha zaidi ulinzi wa anga la Tanzania.
- Amesema kwa kiasi kikubwa rada hiyo pamoja na zile zitakazojengwa Mwanza, Songwe na Kilimanjaro zitasimamiwa na TCAA ikiwamo kuziongoza ili kuhakikisha ulinzi unaimarishwa zaidi.
- Jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo wa rada liliwekwa Aprili 2, 2018 na Rais John Magufuli na utagharimu Sh67 bilioni zikijumuisha mfumo wa rada uliojengwa katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.
Ad
Rattling wonderful information can be found on blog.?
Your style is unique in comparison to other people I’ve read stuff from. Thank you for posting when you have the opportunity, Guess I will just bookmark this blog.
Very good write-up. I absolutely love this site. Thanks!