MAMA MARIA AKUTANA NA BASHIRU ALLY KATIBU MKUU WA CCM

  • Mjane wa Mwalimu Nyerere Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mama Maria Nyerere amekutana na kuwa na mazungumzo na Ndugu Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  • KM-NA-MAKONGORO
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bahiru Ally kushoto akiwa na Makongoro Nyerere.

    Mama Maria ametumia mkutano huu kumpongeza Ndugu Katibu Mkuu kwa juhudi kubwa ambazo anaendelea kuzifanya za kumsaidia Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukirejesha Chama na Serikali kwenye misingi ambayo baba wa Taifa aliisimamia.

KM-NA-MAMA-MARIA-2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bashiru Ally wa (katikati) akiwa na Mama Maria Nyerere na Makongoro Nyerere alipomtembelea nyumbani kwakwe Msasani jijini Dar Es Salaam
  • Mama Maria kwa umahususi na kwa kupitia kwa Ndugu Bashiru amempongeza Ndugu Magufuli kwa kazi nzuri ya ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 200 kote nchini Tanzania ndani ya kipindi kifupi cha miaka miwili, vituo ambayo vina huduma ya afya timilifu (comprehensive health care).
  • Mama Maria ameeleza vituo hivi vitakuwa mkombozi wa upatikanaji wa huduma za afya hasa kwa mama, watoto na wazee. Katika Mkutano huo Mama Maria ametoa wito kwa CCM kuendelea kuisimamia Serikali na kuimarisha lishe bora kwa watoto, watu wazima na umma ili kujenga Taifa imara na la watu wenye nguvu ya kuendelea kuchapa kazi sambamba na kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu!
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bashiru Ally
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bashiru Ally akiwa na Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwakwe Msasani jijini Dar Es Salaam.
  • Akipokea pongezi hizo Ndugu Bashiru Ally, amemshukuru Mama Maria kwa kuendelea kutujali, kutukumbusha, kutushauri na kutuombea kila anapopata nafasi. Ndugu Bashiru amemjulisha Mama Maria kwamba tarehe 17 na 18 Desemba kutafanyika vikao vya Uongozi vya Taifa, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa ambapo serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Mwaka 2015 – 2020.
  • Huu ni muendelezo wa ziara na mazungumzo ya Ndugu Bashiru Ally na viongozi, makada na wanachama wa CCM ili kupokea ushauri, kubadilishana nao uelewa, mipango, mikakati na taarifa za ujenzi wa Chama.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *