Mwonekano wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma ambalo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 80 na unatarajia kukamilika ifikapo mwezi April, 2019, kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 6.2.

UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI

  • Wakazi wa mkoa wa Mara wanatarajia kuondokana na adha ya kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoani Mwanza, umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka mjini Musoma, baada ya ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kukaribia kukamilika mapema mwakani.
MAHAKAMA-2
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Mahakama-Musoma na wakandarasi wanaojenga Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2.
  • Wakizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya wakazi wa mji wa Musoma Mary Mohamed na Happy Mjito, wamesema kuwa hivi sasa wanatumia fedha nyingi kufuatilia haki zao Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza hali inayowafanya wengi wao kukata tamaa kufuatilia kesi zao hivyo kupoteze haki zao
  • “Ukikata rufaa ya kesi unaambiwa uende Mwanza wakati hata Mahakama Kuu yenyewe ya Kanda ya Mwanza hatuijui mahali ilipo, sasa tunafurahi kwamba tutakuwa tumiendesha kesi zetu hapa hapa Musoma” alisema Bi. Happy Mjito
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji,
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzo wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
  • Akielezea hatua ya ujenzi wa Mahakama hiyo Kuu Kanda ya Musoma ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6 nukta 2, Wakala wa Mkandarasi anaye jenga Mahakama hiyo, Kampuni ya DF Mistry, Mhandisi Uday Dadrawalla, ameiambia timu hiyo ya Wizara ya Fedha na Mipango inayofuatilia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mkoani Mara kwamba ujenzi huo umefikia asilimia 80.
  • “Mkataba wetu unaonesha kuwa tunatakiwa kukabidhi jengo ifikapo tarehe 21 mwezi Mei, 2019 lakini kwa kasi tunayokwenda nayo tutakabidhi jengo hili mapema zaidi Mwezi April, 2019” alisema Mhandisi Dadrawalla.
  • Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama Kuu Nchini ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele iliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 hivyo utekelezaji wake ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021, hususani katika eneo la Utawala Bora.(Benny Mwaipaja, WFM)
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *