“SERIKALI YETU INATUJALI NA KUTUPENDA SANA” – DIAMOND PLATNUMZ

 

  • Afanya mahojiano na waandishi wa habari jijini Nairobi.
  • Azungumzia tatizo lililotokea katika onesho la Mwanza na kukiri kuwa yeye na wasanii wenzake walikosea na serikali imewasikiliza na kuwasamehe.
BARAZA LA SANAA LA TAIFA NA WASAFI
Naseeb Abdul – Diamond Platnumz amewaeleza waandishi nchini Kenya kuwa baada ya kukiri na kujutia makosa yao ( Yeye Diamond na msanii mwenzake wa WCB Raymond Mwakyusa – Rayvan) na serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limempunguzia adhabu na kuwaruhusu kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao za sanaa. Aidha Diamond ameipongeza serikali kwa kuwajali na kuwathamini wasanii huku ikiwarudisha katika mstari mara zote wanapotereza au kukiuka taratibu za kufanya kazi za sanaa nchini. Pichani ni Katibu Mtendaji wa BASATA akiwa na wasanii wa WCB wakiwa katika moja ya mikutano na waandishi wa habari kufafanua mambo kadhaa katika shughuli za burudani nchini.
  • Aeleza taratibu walizoelekezwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kumaliza kosa walilofanya na namna wanavyolitekeleza.
  • Sasa Wasafi Festival 2018 kuendelea na ratiba yake ya kutoa burudani jijini Nairobi na Mombasa.
  • Aelezea namna alivyoonana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mzee Jakaya Kikwete na ushauri aliompa.
Diamond Platnumz na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mzee Jakaya Kikwete.jpg
Diamond Platnumz katika mkutano wake na waandishi wa habari nchini Kenya amesema Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mzee Jakaya Kikwete amemshauri mambo mengi muhimu ikiwemo kuoa kwa maana tayari amefikisha umri unaotosha kuanzisha familia yake.
  • Amshukuru pia (Mzee Kikwete) kwa kuchangia nchi yetu kupata Rais Magufuli ambaye ni Rais bora anayeleta maendeleo ya kasi Tanzania ambapo amekiri maendeleo sasa yanaonekana.
RAIS WANGU MZALENDO
Msanii Diamond Platnumz amemsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ni Rais bora na anailetea maendeleo ya kweli Tanzania. Diamond amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari nchini Kenya ambapo alimpongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mzee Jakaya Kikwete kwa kushiriki kupatikana kwa rais bora na sasa Tanzania miradi mingi na mikubwa ya maendeleo inatekelezwa na kukamilika kwa ufanisi mkubwa.
  • Amekanusha kuwa hatumiki kisiasa na tukio la onesho la Wasafi Festival 2018 jijini Mwanza halifanani na msigano wa mwanamuzi Bobby Wine wa Uganda na serikali ya nchi hiyo.

fuatilia sehemu ya mkutano wa Diamond na wasanii wenzake mbele ya waandiahi wa habari nchini Kenya kwa kubofya link hii:-

Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI YA CANADA YATOA FEDHA ZA KITANZANIA BILIONI 90 KWA AJILI YA UJENZI WA MRADI WA VYUO VYA UALIMU NCHINI

Kiasi cha fedha za kitanzania bilioni 90 zimetolewa na Serikali ya Canada kupitia mradi wa  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *