Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa

MIKOA 11 VINARA KWA MABARAZA YA BIASHARA

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ameitaja mikoa 11 ambayo ilianzisha mabaraza ya Biashara na hadi sasa yako hai na kubainisha kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo la kuanzisha mabaraza hayo tu lakini utendaji wa Mabaraza hayo umekuwa siyo endelevu.
Andrew Mhina akiwasilisha taarifa ya utekelezaji
Andrew Mhina akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo mkoani Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
  • Waziri Mhagama ameitaja Mikoa hiyo 11 ambayo Mabaraza yake yako hai hadi sasa kuwa ni Dodoma, Kigoma, Tanga, Geita, Morogoro, shinyanga, Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Songwe na Mbeya. Aidha, Mhagama amebainisha kuwa Mikoa mingine ambayo mabaraza yake hayafanyi vikao inakiuka Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 unaosisitiza kuanzishwa kwa mabaraza hayo na utendaji wake kuwa endelevu.
  • Akiongea wakati wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma, Waziri Mhagama alifafanua kuwa Dhumuni kuu la kuanzisha mabaraza ya biashara hususani katika ngazi ya wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali na Sekta Binafsi katika kila ngazi ya utawala, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa ajili ya kukuza sekta binafsi ambayo ndio muhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.
  • “Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya Baraza la Taifa la Biashara katika ngazi ya Taifa lakini katika ngazi ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili kupunguza kero za wafanya biashara na wawekezaji” Amesema Mhagama
JENISTER
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akisisitiza jambo wakati alipokutana na wajumbe wa Baraza la Biashara Mkoa wa Kigoma, wakati alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, Katibu Tawala wa mkoa huo, Rashid Mchata na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga.
  • Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati Waziri Mhagama alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Mkoa la Biashara, Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga , Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Samson Anga na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Rashid Mchata, walieleza kuwa kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC), wameweza kuimarisha mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi kupitia Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya.
  • Naye Mratibu wa Mradi huo, Andrew Mhina alibainisha kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha kuwa unaboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji nchini tayari kwa kushirikiana Baraza la Taifa la Biashara wameandaa mwongozo wa Majadiliano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuyajengea uwezo Mabaraza ya Mikoa yaweze kuwa endelevu na yenye ufanisi.
  • Baraza la Taifa la Biashara lilianzishwa kwa Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 39 la tarehe 28 Septemba 2001. Baraza hilo ni jukwaa la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, na lengo kuu la Baraza ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa njia ya majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ad

Unaweza kuangalia pia

DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI KATIKA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na …

Oni moja

  1. Hongera sana Mh. Waziri kwa taarifa hii muhimu inayotoa taswira ya utekelezaji wa maelekezo ya Mh.Rais wetu pendwa kwa waraka wake namba 1. 2001 ambao binafsi naona ulenga kabisa kusaidia kukuza mahusiano mema mema baina ya Serikali na Wafanya biashara ili kunogesha mahusiano na kuboresha ulipaji mapato ya Serikali bila ujanja ujanja.
    Kwa mustakabli huo nimeshangazwa na utekelezaji wa Agizo la Mkuu wa Nchi kwani hapa umetaja mikoa 11,tukishuka chini katika wilaya hali inaweza kuwa mbaya zaidi na sina hakika pia na huko kwa ndugu zetu Visiwani Zanzibar hali ikoje.
    Kimsingi nafikiri tunapaswa kuchukua hatua kwa umoja wetu kama watumishi wa Uma kwa kuwa hatua za kukaa pamoja kujadiliana kwa uwazi kunasaidia sana kuleta Tija na kuchochea upatikanaji wa majibu sahihi ambayo hayataleta malalamiko kwa kuwa ni shirikishi mf,mwenendo wa TRA katika Ukusanyaji mapato kwa kutumia mtutu ambapo kulimuibua Mh.RC Gambo wa Arusha na kukemea kwa nguvu zote utaratibu huo wa vitisho na wakizamani.
    Mwisho,naona haja kubewwa kabisa ya kusikiliza kilio cha muda mrefu cha maafisa biashara nchini ambao kimsingi ni kiama wamesahaulika kabisa katika mustakabali wa utendaji wao wa kazi na majukumu yao.
    Maafisa biasjhara wamekuwa wahanga wa matukio ya ukusanyaji mapato,utoaji wa leseni na kuachwa nyuma sana kimuundo na kiutumishi pamoja na jitihada mbalimbali walizofanya kutaka kujiongeza wamekwama sasa sijui hiyo tija ya mabazara nayo itapatikanaje kama kiungonmchezaji ameachwa nyuma.
    Nakupongeza Mh.Waziri kutanabaisha haya
    +255789646064

Leave a Reply to PRIVANUS KATINHILA Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *