Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage (anayefuata kushoto) wakifurahi pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) mara baada ya kuzindua picha ya jengo la Maji linalotarajiwa kumalizika Februari 2020.

DAWASA YAKABIDHIWA JENGO, WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia miradi ya maji kwa umakini mkubwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akimkabidhi mikataba ya makubaliano ya uendeshaji wa jengo la maji lililokuwa chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kupewa DAWASA kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati). Pembeni ni Mjenzi wa jengo hilo wa kampuni ya CCECC.
  • Amewataka DAWASA kuhakikisha kufikia 2020 asilimia 85 ya vijijini na asilimia 95 ya mijini inapata maji safi na salama.
  • Mkumbo amesema hayo wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya jengo la Maji lililopo Ubungo jijini Dar es Salaama na linalotarajiwa kumalizaika Februari 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya mkandarasi msahauri wa jengo hilo.
  • Utiaji wa saini hiyo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.
  • Akizungumza baada ya utiaji wa saini, Mkumbo amesema DAWASA lazima wahakikishe wanasimamia mapato ili kuweza kuendeleza miradi ya maji ili wananchi waweze kufaidika.
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa DAWASA kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.
  • Amesema, hafla ya leo sio ya kukabidhiwa jengo tu ila wanatakiwa kusimamia mradi wa Kidunda, visima vya Kimbiji Mpera pamoja na kuwaunganishia wateja wapya.
  • Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi Mwamunyage amesema changamoto kubwa iliyokuwepo katika mamlaka hiyo ni maeneo ya kufanyia kazi ila baada ya kukabidhiwa jengo hilo wanaamini kwa sasa kazi zitafanyika kwa wakati.
  • Amesema, kwa sasa DAWASA wanajiendesha wenyewe kwa mapato ya ndani na watasimamia mpaka kumalizika Februari 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Picha na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.
  • Naye Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Luhemeja amewashukuru Wizara kwa kuwakabidhi jengo hilo lenye ghorofa 15 kwa ajili ya kuweka ofisi na itawasadia kufanya kazi kwa uharaka zaidi na ameahidi kuwa jengo hilo litakamilika kwa wakati kwani tayari ameshamuagiza Mkurugenzi wa Fedha kuanza kufanya malipo.
  • Pia ameeleza kuwa kwa sasa DAWASA ndani ya miezi mitatu wameweza kufikia malengo ya kufikia Bilioni 10 kwa mwezi katika ukusanyaji wa maji ila wamejizatiti kwa mwaka huu kufikia malengo ya serikali ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini kabla ya 2020 ikiwemo na kupunguza mivujo kwa asilimia 25.
Ad

Unaweza kuangalia pia

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LA PITISHA BAJETI YA BILIONI 170.9 KWA MWAKA FEDHA 2020/ 2021

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, katika Mkutano wake maalumu wa Baraza …

Oni moja

  1. Hakika hii ni hatua muhimu na yafaa iungwe mkono na Watanzania wote.Serikali ya Awamu ya Tano chini ya mzalendo namba moja Rais Dkt.John Magufuli inatekeleza vilivyo mageuzi yenye matokeo chanya kwa umma wote.

Leave a Reply to Godfrey Ismaely Nnko Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *