UJENZI WA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA WASHIKA KASI

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua amewaasa wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa za kazi za ujenzi zinazoendelea katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.
Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati unaoendelea jijini Dodoma . Wanaosikiliza ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (wa pili kushoto) na Wajumbe wa Kamati ya Ujenzi ya Wizara ya Nishati.
  • Katibu Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dodoma baada ya kukagua kazi ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati ambapo aliambatana na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Haji Janabi pamoja na wajumbe wa Kamati ya ujenzi huo wakiongozwa na Katibu wa Kamati, Maseke Mabiki.
  • Akiwa katika eneo hilo la ujenzi, Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amemweleza Katibu Mkuu kuwa, kazi za ujenzi zinaendelea usiku na mchana lakini kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa vibarua wa kutosha watakaoweza kuf anya kazi muda wote.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (aliyenyoosha mkono) akiangalia jinsi kazi za ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati unavyoendelea katika Mji wa Serikali jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga na kushoto kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Haji Janabi.
  • Ameeleza kuwa, ili kuweza kumaliza ujenzi wa jengo hilo ndani ya wakati wameagiza vibarua wengine kutoka Dar es Salaam na Arusha ili kuongeza nguvu kazi.
  • Kuhusu suala hilo, Dkt. Mwinyimvua  pamoja na kutoa wito kwa wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa hizo, ameeleza kuwa atawasiliana na Mamlaka mbalimbali ili kuweza kufanya jitihada za uhamasishaji.
  • Kuhusu ujenzi wa jengo hilo la Wizara, ameeleza kuwa ameridhishwa na kazi za ujenzi zinazoendelea ambapo kwa sasa NHC wamefunga taa zinazowawezesha kufanya kazi kwa masaa 24.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *